003-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 003: وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

An-Nisaa 003-Na mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu kwa mayatima

 

 

وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا ﴿٣﴾

Na mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu kwa mayatima; basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne. Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea kudhulumu [

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka kumzungumzia Bwana mmoja alimuoa binti ambaye ni yatima aliyekuwa akimlea na kumsimamia, kwa sababu hakuwa na mtu wa kumsimamia. Huyo bwana hakumuoa kwa sababu ya kumpenda kwani alikuwa haamiliani naye vizuri. Akamuoa kwa sababu yatima huyo alikuwa ana (mali ya) shamba la mitende. Hapo ikateremka Aayah hii.” [Hadiyth ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share