088-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 088: فَمَا لَكُمْ فِي الْمُنَافِقِينَ فِئَتَيْنِ وَاللَّـهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa     088-Basi mna nini mmekuwa makundi mawili kuhusu wanafiki…

فَمَا لَكُمْ فِي الْمُنَافِقِينَ فِئَتَيْنِ وَاللَّـهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوا ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهْدُوا مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ ۖ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿٨٨﴾

Basi mna nini mmekuwa makundi mawili kuhusu wanafiki; na Allaah Amewageuza (warudie ukafiri) kwa sababu ya waliyoyachuma. Je, mnataka kumwongoa ambaye Allaah Amempotoa? Na aliyepotozwa na Allaah basi hutompatia kamwe njia (ya kumwongoa).(4:88).   

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kuwazungumzia baadhi ya watu ambao walikuwa wametoka pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba zake kwenda katika vita vya Uhud. Wakarejea nyuma na hawakuungana na wenzao. Pakawa katika Swahaba, kuna makundi mawili; kundi moja likawa linasema tuwapige vita! Na kundi jingine likawa linasema hapana! Hapo ikateremka Aayah hii:

فَمَا لَكُمْ فِي الْمُنَافِقِينَ فِئَتَيْنِ وَاللَّـهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوا ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهْدُوا مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ ۖ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿٨٨﴾

Basi mna nini mmekuwa makundi mawili kuhusu wanafiki; na Allaah Amewageuza (warudie ukafiri) kwa sababu ya waliyoyachuma. Je, mnataka kumwongoa ambaye Allaah Amempotoa? Na aliyepotozwa na Allaah basi hutompatia kamwe njia (ya kumwongoa).(4:88).   

 [Amehadithia Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه)   na kupokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]  

Sababun-Nuzuwl:

Pia Sababun-Nuzuwl: Al-‘Awf (رضي الله عنه)  amehadithia kwamba Aayah hii imeteremshwa kuhusu baadhi ya watu wa Makkah ambao walisema wameingia Uislamu lakini huku wakiwaunga mkono washirikina. Walipokwenda Makkah kutimiza mahitaji yao wakaambizana: “Tutakapokutana na Maswahaba wa Muhammad hakutakuwa na madhara yoyote upande wetu.” Waumini walipopata khabari kwamba watu hao wameenda Makkah, wakasema baadhi yao: “Twendeni kwa waoga hao tuwaue kwa sababu wanawaunga mkono maadui zenu dhidi yenu!” Lakini kundi jingine la Waumini wakasema: “Subhaana Allaah! Mnataka kuua watu wanaosema kama mlivyosema kwa sababu tu hawakuhajiri au kuacha ardhi yao? Kwani inaruhusiwa kumwaga damu na kutaifisha mali yao katika hali hii?” Basi wakagawanyika makundi mawili, na wakati huo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa nao na hakukataza kundi lolote kuhusu mabishano yao. Hapo Allaah Akateremsha:

فَمَا لَكُمْ فِي الْمُنَافِقِينَ فِئَتَيْنِ وَاللَّـهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوا ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهْدُوا مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ ۖ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿٨٨﴾

Basi mna nini mmekuwa makundi mawili kuhusu wanafiki; na Allaah Amewageuza (warudie ukafiri) kwa sababu ya waliyoyachuma. Je, mnataka kumwongoa ambaye Allaah Amempotoa? Na aliyepotozwa na Allaah basi hutompatia kamwe njia (ya kumwongoa.(4:88).   

[Ibn Abiy Haatim Tafsiyr Ibn Kathiyr]

Share