100-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 100: وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يَجِدْ فِي الْأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
An-Nisaa 100-Na anayehajiri katika Njia ya Allaah atapata katika ardhi…
وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يَجِدْ فِي الْأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً ۚ وَمَن يَخْرُجْ مِن بَيْتِهِ مُهَاجِرًا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ يُدْرِكْهُ الْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٠﴾
Na anayehajiri katika Njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia kujihifadhi na wasaa (wa kila kitu). Na atakayetoka nyumbani kwake akiwa ni mwenye kuhajiri kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, kisha mauti yakamfikia, basi ujira wake umehakikika kwa Allaah. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. (4:100).
Sababun-Nuzuwl:
Ilipoteremka Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) :
إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ
Hakika wale ambao Malaika wanawafisha, hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao…(4:97),
palikuwepo mtu mmoja Makkah akiitwa Dhwamrah. Yeye alikuwa ni mgonjwa na akaiambia familia yake: “Nitoeni Makkah kwani nahisi joto kali la maradhi.” Familia yake wakamuuliza: “Tukupeleke wapi?” Akaashiria kwa mkono wake kuwa wampeleke Madiynah. Hapo ikateremka Aayah hii:
وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يَجِدْ فِي الْأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً ۚ وَمَن يَخْرُجْ مِن بَيْتِهِ مُهَاجِرًا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ يُدْرِكْهُ الْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٠﴾
Na anayehajiri katika Njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia kujihifadhi na wasaa (wa kila kitu). Na atakayetoka nyumbani kwake akiwa ni mwenye kuhajiri kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, kisha mauti yakamfikia, basi ujira wake umehakikika kwa Allaah. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. (4:100).
[Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) na imepokelewa na Ibn Jariyr]