093-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Maaidah Aayah 093: لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا إِذَا مَا اتَّقَوا
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-Maaidah 093-Hakuna lawama juu ya wale walioamini na wakatenda mema…
لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا إِذَا مَا اتَّقَوا وَّآمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ثُمَّ اتَّقَوا وَّآمَنُوا ثُمَّ اتَّقَوا وَّأَحْسَنُوا ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿٩٣﴾
Hakuna lawama juu ya wale walioamini na wakatenda mema katika vile walivyokula (kabla ya kuharimishwa) ikiwa watakuwa na taqwa na wakaamini na wakatenda mema; kisha wakawa na taqwa na wakaamini, kisha wakawa na taqwa na wakafanya ihsaan. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan. (5:93). [Amehadithia Anas (رضي الله عنه), imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii imeteremshwa baada ya kuteremshwa Aayah za uharamisho wa pombe moja kwa moja (5:90-91). Kisha baadhi ya Swahaba wakasema kuwa watu wengi wamefariki wakiwa wana pombe matumboni mwao, wakataka hukmu yake, hapo ikateremka Aayah hii: