108-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Maaidah Aayah 108: ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يَأْتُوا بِالشَّهَادَةِ عَلَىٰ وَجْهِهَا أَوْ يَخَافُوا أَن تُرَدَّ أَيْمَانٌ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-Maaidah 108-Hivyo inaelekea zaidi ya kwamba watatoa ushahidi kama…
ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يَأْتُوا بِالشَّهَادَةِ عَلَىٰ وَجْهِهَا أَوْ يَخَافُوا أَن تُرَدَّ أَيْمَانٌ بَعْدَ أَيْمَانِهِمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاسْمَعُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿١٠٨﴾
Hivyo inaelekea zaidi ya kwamba watatoa ushahidi kama ipasavyo au watakhofu visije vikaletwa viapo (vingine) baada ya viapo vyao. Na mcheni Allaah na sikizeni! Na Allaah Haongoi watu mafasiki. [Al-Maaidah (5:106-108)]
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii imeteremshwa pamoja na Aayah mbili kabla yake (5:106-107) pale bwana mmoja katika Baniy Sahm alitoka pamoja na Tamiym Ad-Daariy na ‘Adiyy. Kisha katika msafara wao akafariki huyu mtu ambaye ni katika Baniy Sahm, na walikuwa katika kijiji ambacho hakuna Muislamu. Pale waliporejea akina Tamiym na vitu vyake alivyoviacha baada ya kufariki, walikikosa chombo kimoja cha fedha ambacho kimezibiwa kwa dhahabu. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaapisha. Kisha baada ya hapo walikuja kukipata kile chombo Makkah. Wakasema wale waliokipata huko Makkah kwamba: Tulikinunua kwa ‘Adiy na Tamiym. Wakasimama watu wawili katika ndugu wa yule As-Sahm wakaapa na wakasema kumuambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa ushahidi wetu ni bora kuliko ushahidi wao, na kwamba hao ni waongo wanamsingizia Tamiym na ‘Adiy na kuwa hicho chombo si cha huyo ndugu yao bali ni cha jamaa yao wenyewe. Hapo zikateremka Aayaat hizi:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا شَهَادَةُ بَيْنِكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ حِينَ الْوَصِيَّةِ اثْنَانِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ أَوْ آخَرَانِ مِنْ غَيْرِكُمْ إِنْ أَنتُمْ ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَأَصَابَتْكُم مُّصِيبَةُ الْمَوْتِ ۚ تَحْبِسُونَهُمَا مِن بَعْدِ الصَّلَاةِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ إِنِ ارْتَبْتُمْ لَا نَشْتَرِي بِهِ ثَمَنًا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۙ وَلَا نَكْتُمُ شَهَادَةَ اللَّـهِ إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الْآثِمِينَ ﴿١٠٦﴾
Enyi walioamini! Ushahidi uliofaradhishwa kati yenu ni wa watu wawili waadilifu wakati wa kuandika (au kutamka) usia anapohisi mmoja wenu dalili za kukurubia kufa, au wawili wengineo wasiokuwa nyinyi pale mnapokuwa safarini ukakufikeni msiba wa mauti. Muwazuie baada ya Swalaah, na waape kwa Allaah mkitilia shaka, (waseme): Hatutovibadilisha (viapo vyetu) kwa thamani yoyote ile japo akiwa ni jamaa yetu wa karibu. Na wala hatutoficha ushuhuda wa Allaah, kwani hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye kutenda dhambi.
فَإِنْ عُثِرَ عَلَىٰ أَنَّهُمَا اسْتَحَقَّا إِثْمًا فَآخَرَانِ يَقُومَانِ مَقَامَهُمَا مِنَ الَّذِينَ اسْتَحَقَّ عَلَيْهِمُ الْأَوْلَيَانِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ لَشَهَادَتُنَا أَحَقُّ مِن شَهَادَتِهِمَا وَمَا اعْتَدَيْنَا إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠٧﴾
Ikigundulikana kwamba hao wawili wana hatia ya kukhini, basi wawili wengine wanaostahiki kudai haki ki-shariy’ah, na walio karibu zaidi (na mrithiwa) wasimame mahala pao, kisha waape kwa Allaah: Bila shaka ushahidi wetu ni wa kweli zaidi kuliko ushahidi wa wawili wao; nasi hatukufanya taksiri, kwani bila shaka hapo sisi tutakuwa miongoni mwa madhalimu.
ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يَأْتُوا بِالشَّهَادَةِ عَلَىٰ وَجْهِهَا أَوْ يَخَافُوا أَن تُرَدَّ أَيْمَانٌ بَعْدَ أَيْمَانِهِمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاسْمَعُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿١٠٨﴾
Hivyo inaelekea zaidi ya kwamba watatoa ushahidi kama ipasavyo au watakhofu visije vikaletwa viapo (vingine) baada ya viapo vyao. Na mcheni Allaah na sikizeni! Na Allaah Haongoi watu mafasiki. [Al-Maaidah (5:106-108)]. [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما), ameipokea Al-Bukhaariy]
An-Naasikh Wal-Mansuwkh:
Kufutwa hukmu kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
أَوْ آخَرَانِ مِنْ غَيْرِكُمْ
au wawili wengineo wasiokuwa nyinyi (5:106).
Imefutwa baada ya kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِّنكُمْ وَأَقِيمُوا الشَّهَادَةَ لِلَّـهِ ۚ ذَ
na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. [Atw-Twalaaq (65: 2)].