Imaam Ibn Baaz: Vitabu Muhimu Vya Tafsiyr, Hadiyth Na Fiqh
Vitabu Muhimu Vya Tafsiyr, Hadiyth Na Fiqh
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Naomba unieleweshe majina ya vitabu muhimu vya Tafsiyr (ufafanuzi wa maana za Qur-aan), Hadiyth na Fiqh (Falsafa ya Shariy’ah ya Kiislamu).
JIBU:
A-Vitabu muhimu vya Tafsiyr ni pamoja na:
1. Tafsiyr ya Ibn Jariyr
2. Tafsiyr ya Ibn Kathiyr
3. Al-Baghaway
4. Ibn Sa’dy na
5. Al-Shanqiytwiy.
B-Vitabu muhimu vya Hadiyth ni pamoja na:
1. Vitabu viwili Swahiyh vya Hadiyth (yaani Al-Bukhaariy na Muslim)
2. Sunan (mikusanyiko ya Hadiyth ambazo zimefafanuliwa kwa maudhui ya ki-Fiqh) iliyoandikwa na Wakusanyaji Wanne wa Hadiyth (Imaam Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah)
3. Muntaqa Al-Akhbaar
4. ‘Umdat Al-Hadiyth
5. Buluwgh Al-Maraam na
6. Al-Arba’un An-Nawawiyyah na hitimisho za Al-Haafidhw Ibn Rajab. Ni Hadiyth khamsini zilizosimuliwa kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) chini ya jina la Jawami’ Al-Kalim (fupi lakini ni lenye kutosheleza kiufafanuzi).
C-Vitabu muhimu vya Fiqh ni pamoja na:
1. Al-Mughny na Al-Muqni’ ambacho ni cha Mwanachuoni mkubwa, Imaam Abuu Muhammad bin ‘Abdillaah bin Qudaamah (Rahimahu Allaah)
2. Al-Rawdhw Al-Murabba’ Sharh Zaad Al-Mustanqa’ chenye sharh ya Shaykh ‘Abdur-Rahmaan bin Qaasim (Rahimahu Allaahu) na
3. Sharh Al-Muhadhab cha An-Nawawiy (Rahimahu Allaahu).
Allaah Atujaalie mafanikio!
[Fataawa Ibn Baaz, Angalia kwa namba ya Sura, Sura ya 24, Kitabu Kuhusiana Na Tafsiyr, Vitabu Muhimu Vya Tafsiyr]