014-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuhesabiwa Hesabu Nyepesi Siku Ya Qiyaamah
Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Kuomba Kuhesabiwa Hesabu Nyepesi Siku Ya Qiyaamah
اللَّهُمَّ حَاسِبْنِي حِسَابًا يَسِيرًا
Allaahumma haasibniy hisaaban -yasiyraa
Ee Allaah nihesabie hisabu iliyo nyepesi
Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عنها) alimuuliza Rasuli wa Allaah (سبحانه وتعالى) alipomaliza kuisoma du’aa katika Swalaah: “Ipi hesabu iliyo nyepesi?” Akasema: ((Kwamba [Allaah] Atatazama kitabu chake [kilichorekodiwa ‘amali] kisha Amsamehe kwani hakika mwenye kuhojiwa hesabu siku hiyo ee ‘Aaishah ameangamia, na kila kinachomsibu Muumini Allaah عز وجل Humfutia ([dhambi] japo ikiwa ni mwiba umchomao)) [Imaam Ahmad]