034-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuunganishwa Nyoyo, Kusuluhishwa, Kuongozwa Njia Ya Amani, Kuokoka Kiza...
Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Kuomba Kuunganishwa Nyoyo. Kusuluhishwa, Kuongozwa Njia Ya Amani, Kuokoka Na Kiza Na Kuingia Katika Nuru...
اللَّهُمَّ أَلِّفْ بَيْنَ قُلُوبِنَا، وَأَصْلِحْ ذَاتَ بَيْنِنَا، وَاهْدِنَا سُبُلَ السَّلاَمِ، وَنَجِّنَا مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّور، وَجَنِّبْنَا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ، وَبَارِكْ لَنَا فِي أَسْمَاعِنَا، وَأَبْصَارِنَا، وَقُلُوبِنَا، وَأَزْوَاجِنَا، وَذُرِّيَّاتِنَا، وَتُبْ عَلَيْنَا إِنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ، وَاجْعَلْنَا شَاكِرِينَ لِنِعْمَتِكَ مُثْنِينَ بِهَا قَابِلِيهَا وَأَتِمَّهَا عَلَيْنَا
Allaahumma allif bayna quluwbinaa, wa aswlih dhaata bayninaa, wahdinaa subulas-ssalaami, wanajjinaa minadhw-dhwulumaati ilan-nnuwri, wa jannibnal-fawaahisha maa dhwahara minhaa wamaa batwan, wa Baarik-lanaa fiy asmaa’inaa, wa abswaarinaa, wa quluwbinaa, wa azwaajinaa, wa dhurriyaatinaa, watub ‘alaynaa innaka Antat-Tawaabur-Rahiym, waj-’alnaa shaakiriyna lini’matika muthniyna bihaa qaabiliyhaa wa atimmahaa ‘alaynaa
Ee Allaah! Unganisha baina ya nyoyo zetu, na Suluhisha yaliyo baina yetu, na Tuongoze njia za amani, na Tuokoe kutokana na viza Utuingize katika Nuru, na Tuepushe machafu ya dhahiri na ya siri, na Tubarikie katika kusikia kwetu na kuona kwetu, nyoyo zetu, na wake zetu, na vizazi vyetu, na Tupokelee tawbah zetu, hakika Wewe ni At-Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye Kurehemu), na Tujaalie kuwa wenye kushukuru neema Zako, wenye kuzielezea kwa uzuri, wenye kuzipokea (kwa shukrani), na Zitimize kwetu.
[Abuu Daawuwd, Al-Haakim akasema ‘Swahiyh kwa sharti ya Muslim, na ameikubali Adh-Dhahabiy (1/265)]