049-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Ya Kila Shari, Kulipiwa Madeni Na Kinga Ya Ufakiri
Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Kuomba Kinga Ya Kila Shari, Kulipiwa Madeni Na Kinga Ya Ufakiri
Du’aa hii ni miongoni mwa nyiradi za unaingia kitandani kulala.
اللَّهُمَّ رَبَّ السَّمَاوَاتِ السَّبْعِ وَرَبَّ الأَرْضِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ، رَبَّنَا وَرَبَّ كُلِّ شَيْءٍ، فَالِقَ الْحَبِّ وَالنَّوَى، وَمُنْزِلَ التَّوْرَاةِ وَالإِنْجِيلِ وَالْفُرْقَانِ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ كُلِّ شَيْءٍ أَنْتَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهِ، اللَّهُمَّ أَنْتَ الأَوَّلُ فَلَيْسَ قَبْلَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الآَخِرُ فَلَيْسَ بَعْدَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الظَّاهِرُ فَلَيْسَ فَوْقَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الْبَاطِنُ فَلَيْسَ دُونَكَ شَيْءٌ ، اقْضِ عَنَّا الدَّيْنَ وَأَغْنِنَا مِنَ الْفَقْر
Allaahumma Rabbas-samaawatis-sab-‘i wa Rabbal-ardhwi, wa Rabbal-‘Arshil-‘Adhwiym, Rabbanaa wa Rabba kulli shay-in, faaliqal-habbi wan-nnawaa, wa munzilat-Tawraati wal-Injiyli wal-Furqaan. A’uwdhu bika min sharri kulli shay-in Anta aakhidhun binaaswiyatihi. Allaahumma Antal-Awwalu falaysa qablaka shay-un, wa Antal-Aakhiru falaysa ba’-daka shay-un wa Antadhw-Dhwaahiru falaysa fawqaka shay-un, wa Antal-Baatwinu falaysa duwnaka shay-un. Iqdhwi ‘annad-dayna wagh-ninaa minal-faqri
Ee Allaah, Rabb wa mbingu saba na Rabb wa ardhi, na Rabb wa ‘Arsh ‘Adhimu, Rabb wetu na Rabb wa kila kitu, Mpasuaji wa mbegu na kokwa na Aliyeiteremsha Tawraat na Injiyl na Qur-aan. Najikinga Kwako shari ya kila kitu, Wewe Ndiye Mwenye kukamata utosi wake. Ee Allaah, Wewe Ndiye Al-Awwalu (wa Awali hakuna kitu kabla Yako) na Al-Aakhiru (wa Mwisho hakuna kitu baada Yako) na Adhw-Dhwaahiru (Uliye juu hakuna kitu juu Yako), na Al-Baatwinu (Uliye karibu, hakuna kitu kilichokaribu kuliko Wewe), Nilipie madeni yangu na Niepushe na ufakiri.
[Muslim]