063-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Dhidi Ya Jirani Muovu
Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Kuomba Kinga Dhidi Ya Jirani Muovu
063- Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako jirani muovu katika…
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ جَارِ السَّوْءِ فِي دَارِ الْمُقَامِ فَإِنَّ جَارَ الْبَادِيَةِ يَتَحَوَّلُ
Allaahumma inniy a’uwdhu bika min jaaris-saw-i fiy daaril-muqaami fainna jaaral-baadiyati yatahawwalu.
Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako na jirani muovu katika makazi ya kudumu kwani jirani wa jangwani hubadilika badilika kuhama.
[An-Nasaaiy kwa usimulizi ((Jikingeni na jirani muovu…)), As-Silsilatu Asw-Swahiyhah (3943), Swahiyh Al-Jaami’ (2967)]
Ufafanuzi: Makazi ya kudumu: Makazi ya kuthibitika hayabadiliki; watu hubakia hawaondoki kuhama kuhama.