04-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Miji Ambayo Masaa ya kufunga Swawm Ni Marefu Sana
Miji Ambayo Masaa ya kufunga Swawm Ni Marefu Sana
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Tuko katika Mji ambapo jua halizami mpaka saa 3:30 au 4:00 (saa tatu au saa nne) za usiku. Ni lini tunatakiwa tufungue Swawm?
JIBU:
Utafufungua Swawm kufuturu wakati jua linapozama. Maadamu tu mko na mchana na usiku kwa masaa 24, unawajibika kufunga swiyaam, hata kama masaa ni marefu kiasi gani.
[Fataawa Islaamiyah uk. 276, mj. 2]
