06-Shaykh Al-Luhaydaan: Msafiri Wa Mara Kwa Mara Katika Ramadhwaan
Msafiri Wa Mara Kwa Mara Katika Ramadhwaan
Shaykh Al-Luhaydaan
SWALI:
Mimi ni muendesha lori na huendesha kutwa nzima kutoka mji hadi mji. Je, naingia katika hukmu ya masafiri au nalazimika kufunga Swawm ya mwezi wa Ramadhwaan?
JIBU:
Inajuzu mtu kufunga siwyaam hata kama yuko safarini, isipokuwa tu kama mtu atahofia madhara katika afya yake. Maadamu kazi yako hii ni ya kila siku, inajuzu kwako kufunga swiyaam ikiwa kama huhofii madhara. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitoka yeye na Maswahaba wake katika Ramadhwaan wakienda Vitani - Miongoni mwao pako waliokuwa wakifunga swiyaa wala hakuwakataza kama ilivyokuja katika Hadiyth. Anasema mmoja katika Maswahaba: "Tulikuwa tukisafiri pamoja na Nabiy (Swala Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) baadhi yetu tunafunga swiyaam na wengine wanakula - Kulikuwa hakuna tatizo kwa yule aliyefunga, na yule ambaye hakufunga.”
Kwa hiyo hakuna matatizo, bali ni bora zaidi (kwa yule msafiri ambae ndio kazi yake) afunge wakati wa safari isipokuwa tu kama atahofia madhara kwenye afya yake.