08-Imaam Ibn Qudaamah Al-Maqdisiy: Mwanamke Anayelazimishwa Kujimai Wakati Wa Ramadhwaan
Mwanamke Anayelazimishwa Kujimai Wakati Wa Ramadhwaan
Imaam Ibn Qudaamah Al-Maqdisiy
SWALI:
Ikiwa mwanamke atalazimishwa jimai, halazimiki kulipa kafara, bali analazimika kulipa tu siku hiyo?
JIBU:
Muhannaa kasema: "Nilimuuliza Ahmad kama mwanamke aliyebakwa analazimika kulipa siku hiyo. Akasema: "Ndiyo." Pia nikamuuliza kama analazimika kulipa kafara, akasema: "Hapana!"
Maoni haya anakubaliana nayo pia al-Hasan, Ath-Thawriy, Al-Awza'iy na Hanafiyyah.
Kulingana na swali hili, inamuhusu pia mwanamke ambaye kaingiliwa wakati amelala.
Maalik kasema kuhusiana na mwanamke aliyelala: "Ni juu yake kulipa siku hiyo, ila hatolipa kafara. Ama kuhusiana na mwanamke ambaye amelazimishwa kujimai, analazimika kulipa siku hiyo na kutoa kafara.”
Ash-Shaafi'iy, Abuu Ath-Thawriy na Ibnul-Mundhir wanasema ikiwa ataingiliwa jimai kwa matisho, basi wana maoni sawa na sisi.
[Al-Mughniy (4/376) Daar 'Alaam-il-kutub, 1419/1999]