06-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Hukmu Ya Anayefunga Na Kuswali Ramadhwaan Pekee

Hukmu Ya Anayefunga Na Kuswali Ramadhwaan Pekee

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Unasemaje kwa yule mtu ambaye anaswali na kufunga wakati wa Ramadhwaan tu? Wakati Ramadhwaan inakwisha, anaacha kuswali na kufunga?

 

 

JIBU:

 

Kilicho dhahiri kwangu kutokana na dalili, ni kwamba mtu kama huyo anachukuliwa kama ni kafiri kama haswali kabisa. Ama kuhusu yule ambaye anaswali wakati fulani na wakati mwingine haswali,  sidhani kuwa dalili yaonesha kuwa mtu huyo ni kafiri (moja kwa moja).

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Ahadi baina yetu sisi na wao (makafiri) ni Swalaah. Yule atakayeiacha huyo amekufuru.”

Na pia:

"Baina ya mshirikina na shirki ni mtu kuacha Swalaah.”

 

Ndiyo maana nina mashaka ya iymaan ya mtu ikiwa anaswali na kufunga wakati wa Ramadhwaan pekee.  Kama kweli ni Muumini wa kweli, anapaswa kuswali wakati wote ikiwa ni Ramadhwaan na baada ya Ramadhwaan.

 

Kumjua Rabb wake wakati wa Ramadhwaan pekee, ninaingiwa na shaka kutokana na iymaan yake. Hata hivyo sisemi kuwa ni kafiri moja kwa moja, badala yake ninamdhania vizuri na kumuachia suala lake kwa Allaah (‘Azza wa Jalla).

 

 

[Fiqhul-'Ibaadat, uk. 248, Madaar Al-Watwan, 1424]

 

Share