02-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Alipe Siku Ambayo Amepata Maumivu Ya Hedhi Kabla Ya Jua Kuzama?
Alipe Siku Ambayo Amepata Maumivu Ya Hedhi Kabla Ya Jua Kuzama?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, Swawm ya mwanamke ni Sahihi, au ni waajib kwake kulipa siku hiyo, ikiwa anadhani (anahisi) atapata hedhi au yuko na maumivu ya hedhi lakini bila ya yeye kupata chochote kabla ya jua kuzama?
JIBU:
Ikiwa mwanamke aliye msafi anahisi kwamba damu iko njiani au ana maumivu ya hedhi wakati yeye ni mwenye Swawm bila ya yeye kutokwa na kitu kabla ya jua kuzama, Swawm yake ni sahihi. Hana haja ya kulipa siku hiyo ikiwa kama ni Swawm ya waajib, na hatokosa ujira wake ikiwa ni Swawm ya Sunnah.
[Imaam Ibn 'Uthaymiyn - Su-alaat ‘an Ahkaamil-Haydhw uk. 11]