07-Imaam Ibn ‘Uthyamiyn: Akimeza Maji Bila Kukusudia Kutokana Na Kusukutua Swawm Yake Inabatilika?
Akimeza Maji Bila Kukusudia Kutokana Na Kusukutua Swawm Yake Inabatilika?
Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, Swawm ya mfungaji inabatilika ikiwa atasukutua kinywa au pua na kwa bahati mbaya akameza maji?
JIBU:
Aliyekuwa katika swawm akaukutua kinywa au pua na maji yakamuingia, Swawm yake haibatiliki, kwa kuwa hakukusudia hilo. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:
وَلَـٰكِن مَّا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ ۚ
lakini isipokuwa katika yale yaliyoyakusudia nyoyo zenu [Al-Ahzaab 33;5]
[Imaam Muhammad Swaalih Ibn 'Uthaymiyn - Fiqhul-'Ibaadat, uk. 253]