04-Imaam Ibn ‘Uthyamiyn: Hukmu Ya Aliyeacha Swiyaam Miaka Ya Nyuma

Hukmu Ya Aliyeacha Swiyaam Miaka Ya Nyuma

 

Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI: 

 

Nini hukmu ya Muislamu aliyekuwa hafungi miaka ya nyuma ingawa alikuwa akitimiza fardhi nyingine, na kuacha swiyaam huko kulikuwa bila ya kizuizi au sababu yoyote? Je, Inampasa alipe swiyaam hizo hata baada ya kutubu?

 

 

JIBU:

 

Iliyokuwa sahihi ni kwamba haimpasi kulipa swiyaam za nyuma zilizompita alizokuwa hazifungi baada ya kutubu. Hii ni kwa sababu ‘amali zote za ‘ibaadah kwa Waumini zimewekwa katika muda wake mahsusi uliotajwa.

 

Kwa hiyo, ikiwa mtu atawacha kufanya ‘ibaadah hiyo au kuichelewesha na muda upite bila ya sababu yoyote, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Hatapokea ‘amali hiyo. Na kutokana na hayo, hakuna maana kulipa yaliyompita. Lakini, inampasa atubu kikweli kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na azidishe sana ‘amali njema, na yule mwenye kuomba msamaha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), basi Allaah  Atamsamehe.

 

 

[Imaam Ibn ‘Uthyamiyn - Fataawaa Ramadhwaan - Mjalada 2, Uk 556, Fatwa Namba 539;
Fataawaa  Shaykh Muhammad Swaalih Al-'Uthaymiyn – Mjalada  1, Ukurasa  536]

 

 

Share