01-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Alijimai Bila Ya Kujua Kwamba Alfajiri Imeingia Akaendelea Na Swawm

Alijimai Bila Ya Kujua Kwamba Alfajiri Imeingia Akaendelea Na Swawm

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Alifanya jimai na mkewe katika masaa ya mwisho ya usiku akidhania kuwa wakati wa Alfajiri bado haujaingia. Lakini, baada ya kumaliza, katoka chumbani na kutambua kuwa amefanya kitendo hicho baada ya Alfajiri kuingia. Amesikitika na akaendelea na Swawm.  Lakini anahisi kuwa amefanya dhambi na anauliza nini kinachompasa kufanya kuhusu kufanya kitendo hiki baada ya Alfajiri kuingia?

 

 

JIBU:

 

Kama hali ilikuwa kama ilivyotajwa, basi anatakiwa alipe siku hiyo kama ana hakika kuwa alifanya jimai baada ya kutakiwa ajiepushe na mambo yanayovunja Swawm baada ya kuingia Alfajiri. Na akishalipa siku hiyo, anatakiwa aache huru mtumwa mmoja aliye Muumini. Na ikiwa hawezi basi afunge miezi miwili mfululizo (bila ya kupumzika) na ikiwa hawezi basi alishe masikini sitini (60) au watu wanaohitaji kwa sababu ya dharau yake ya kufanya kitendo hicho bila ya kuhakikisha wakati wa Alfajiri kuingia. Na mke naye anatakiwa kulipa hivyo hivyo isipokuwa ikiwa alilazimishwa kufanya kitendo hicho cha ndoa na mumewe.

 

Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam. 

 

 

[Fataawa Ramadhwaan - Mjalada 2, Ukurasa  615, Fatwa Namba 612; Fataawa Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah Wal-Iftaa - Fatwa Namba 10676]

 

 

 

Share