05-Imaam Ibn Baaz: Mke Alipe Kafara Ikiwa Alijimai Na Mumewe Siku Za Ramadhwaan?
Mke Alipe Kafara Ikiwa Alijimai Na Mumewe Siku Za Ramadhwaan?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Mtu alijimai (kitendo cha ndoa) na mkewe katika siku ya Ramadhwaan na kwa hivyo akafunga swiyaam kama ni kafara miezi miwili mfululizo. Sasa mkewe anatakiwa kufanya lolote? Allaah Akulipeni.
JIBU:
BismiLLaah. Himdi zote ni za Allaah Pekee.
Yale yale yanayompasa yeye mke ni sawa na yanayompasa mumewe ikiwa alifanya kitendo hicho kwa pendekezo lake mwenyewe na hakulazimishwa.
Na ikiwa ni shida kwake swiyaam ya miezi miwili mfululizo, basi alishe masikini sitini au kuwalisha wanaohitaji. Kila mmoja amlishe pishi moja (sawa na vibaba vinne au 3kg) .
Lakini kama alilazimishwa na kupigwa basi hatakiwi kulipa lolote na dhambi zitakuwa ni za mume pekee. Lakini kama alifanya kwa mapendekezo basi anatakiwa alipe kafara sawa sawa na mumewe.
[Imaam Ibn Baaz - Fataawaa Ramadhwaan – Mjalada 2, Ukurasa 610, Fatwa Namba 605 -Majmuw' Fataawaa libni Baaz - Mjalada 3, Ukurasa 200]