03-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Swiyaam Za Siku Sita Za Shawwaal Ni Lazima Kuanza Baada Tu Ya 'Iydul-Fitwr?
Swiyaam Za Sita Shawwaal Ni Lazima Kuanza Baada Tu Ya 'Iydul-Fitwr?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Je, swiyaam za Sitta Shawwaal ni lazima kuanza kufunga siku ya pili tu baada ya 'Iydul-Fitwr au inaruhusiwa kuanza baada ya siku chache?
JIBU:
Si lazima kwa mtu kuanza Swiyaam baada ya siku ya kwanza ya 'Iyd, bali anaweza kuanza siku ya pili au ya tatu au hata zaidi ya masiku ndani ya mwezi huo wa Shawwaal.
Vile vile anaweza kufunga moja kwa moja bila ya kusita au kufunga na kupumzika kwani jambo hili ni dhahiri kuwa si fardhi bali ni Sunnah.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil Buhuwth Al-‘Ilmiyyaa Wal Iftaa Fatwa 3475 – Fataawaa Ramadhwaan – Majalada 2, Ukurasa 693, Fatwa Namba 698]