Pakoras (Bajia) Za Bilingani Na Viazi Kwa Salsa Ya Uwatu
Pakoras Bajia Za Bilingani, Viazi Kwa Salsa Ya Uwatu
Vipimo
Bilingani 1 katakata vipande vidogodogo
Viazi 2 katakata vipande vidodogo vyembamba
Kitunguu 1 katakata slice za kiasi
Kotmiri msongo (bunch) moja ndogo katakata
Pilipili mbichi 1 katakata ndogo ndogo
Jira/bizari nzima/cumin 1 kijiko cha chai
Chumvi kijiko 1 cha chai
Haldi/bizari ya manjano (turmeric) ½ kijiko cha chai
Uwatu wa unga (methi/fenugreek) ½ kijiko cha chai
Unga wa dengu kikombe 1
Maji ½ kikombe
Mafuta ya kukaangia
Vipimo Vya Salsa
Pilipili kubwa tamu (capsicum)
Nyanya 2
Thomu (saumu/garlic) chembe 3
Pilipili mbichi 2
Uwatu (methi/fenugreek) 1 kijiko cha chai
Siki au ndimu vijiko vya kulia
Chumvi kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya vizuri vitu vyote vya bajia katika bakuli.
- Weka mafuta katika karai yaache yashike moto. Chota kwa kijiko cha kulia au kwa mkono mchanganyiko wa bajia ukaange katika mafuta.
- Kaanga mpaka zigeuke rangi.
- Epua uchuje mafuta kwenye chujio kisha weka katika kitchen tissues zizidi kuchuja mafuta.
- Panga katika sahani zikiwa tayari.
Salsa Ya Nyanya Pilipili Tamu Na Uwatu
- Katakata vitu katika mashine ya kusagia (blender) usage vizuri.
- Mimina katika bakuli utolee la pakoras (bajia)
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)