11-Imaam Ibn Baaz na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Je, I’tikaaf Inasihi Katika Misikiti Mingineyo Isiyokuwa Ile Mitatu?
Je, I’tikaaf Inasihi Katika Misikiti Mingineyo Isiyokuwa Ile Mitatu?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
11-Je, I’tikaaf Inasihi Katika Misikiti Mingineyo Isiyokuwa Ile Mitatu? (Masjid Al-Haraam (Makkah), Masjid An-Nabawiy (Madiynah), Masjid Al-Aqswaa (Palestina).
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
a. I’tikaaf inasihi katika Misikiti mingineyo isiyokuwa katika mitatu isipokuwa ikiwa mtu ametoa nadhiri kutekeleza I’tikaaf katika Misikiti mitatu basi hapo inamlazimu atekeleze I’tikaaf humo ili atimize nadhiri yake.
b. Isipokuwa ikiwa haiswaliwi Swalaah ya jamaa’ah humo basi I’tikaaf haisihi kutekelezwa humo.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/444)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Inajuzu I’tikaaf katika Misikiti mingineyo isiyokuwa ile mitatu na ikiwa Hadiyth hii ni swahiyh “Isifanywe I’tikaaf isipokuwa Misikiti mitatu”, basi iliyokusudiwa ni kwamba I’tikaaf humo ni yenye ukamilifu na bora zaidi.
[Majmuw’ Al-Fataawa 20/160)]