18-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kutiya Niyyah I’tikaaf Makumi Ya Mwisho Ramadhwaan Kisha Kutoka Usiku Wa Mwisho
Kutiya Niyyah I’tikaaf Makumi Ya Mwisho Ramadhwaan Kisha Kutoka Usiku Wa Mwisho
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
18. Aliyetia Niyyah Kuingia I’tikaaf Makumi Ya Mwisho Katika Ramadhwaan Kisha Akataka Kutoka Usiku Wa Mwisho; Je, Kuna Makosa Juu Yake?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Ikiwa hakuwekea nadhiri na kukata kwake ni katika siku ya mwisho au kabla yake, basi hakuna dhambi juu yake. Lakini linalopendekezeka zaidi ni akamilishe ili apate kutekeleza Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwani yeye hakuwa akitoka kwenye I’tikaaf yake mpaka iingie mwezi wa Shawwaal.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/184)]