Shaykh 'Abdul-'Aziyz Aal-Shaykh: Hukumu Ya Kunyoa Au Kupunguza Ndevu Na Isbaal

 

Hukumu Ya Kunyoa Au Kupunguza Ndevu Na Isbaal

 

´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal-Shaykh (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Naomba muelekezo katika haki kwa kuwa nimechanganyikiwa, kuhusiana na suala la kunyoa ndevu na Isbaal? Ipi hukumu ya kunyoa ndevu

 

 

JIBU:

 

Kuzinyoa ni Haramu, na kuzifupisha ni Haramu. Na Sunnah ni kuziacha ndevu kama zilivyo kwa maadhimisho ya uongofu wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Usimjali yeyote anayesema kuwa kufupisha inajuzu au wanaojaribu kushawishi kukata ndevu kwa njia yoyote kuwa inajuzu, hata akikwambia kuwa ni mtu mwenye elimu, na yeye kusema kweli ni mtu asiyekuwa na elimu. Sunnah inamgusa kila mtu.

 

Na Isbaal ya vazi (kuvaa nguo ikavuka mafundo ya miguu) ni Haramu.

 

“Chenye kuvuka chini ya mafundo ya miguu katika vazi hupelekea motoni” [Al-Bukhaariy]

 

"Atayeteremsha vazi lake kwa kiburi, Allaah hatomtazama siku ya Qiyaamah." [Tirmidhiy]

 

“Watu watatu Hatowasemesha Allaah siku ya Qiyaamah, na Hatowatazama, na Hatowatakasa, na watapata adhabu iumizayo; (Hao ni) al Musbil – Mwenye kuburuza nguo yake, mwenye kutoa na kukizungumzia alichokitoa, Na mwenye kuuza bidhaa zake kwa kutumia kiapo cha uongo” [Muslim]

 

 

[´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal-Shaykh]

 

 

Share