Shaykh 'Abdul-Muhsin Al-'Abbaad: Je, Anayenyoa Ndevu Anapata Madhambi?
Je, Anayenyoa Ndevu Anapata Madhambi?
Shaykh ´Abdul-Muhsin Al-´Abbaad (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Je, Anayenyoa ndevu zake anapata madhambi kwa kuzinyoa?
JIBU:
Na'am, anapata madhambi. Kwa kuwa kufuga ndevu ni wajibu na kuzinyoa ni haramu.
Dalili ya hilo, imekuja katika Sunnah kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth nyingi anaamrisha ndani yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) kufuga ndevu, kuzirefusha, kuziachia na kuziacha kwa wingi.
Matamshi yote haya yamekuja kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam). Na imekuja vilevile jitofautisheni na washirikina na jitofautisheni na majusi. Na imekuja vilevile:
”Allaah Kawalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake. Na wanawake wanaojifananisha na wanaume.”
Na ni jambo linalojulikana kule mwanaume kunyoa ndevu zake, anakuwa amejifananisha na wanawake ambao Allaah Kawaumba bila ya ndevu usoni. Mwenye kufanya hivyo atakuwa anapata madhambi na katumbukia katika maasi, kwa kwenda kwake kinyume na maamrisho na (vilevile) kujifananisha kwake na wanawake.
[http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=9636]