17-Fatwa: Zipi Zinapaswa Kutangulizwa Swiyaam Za Nadhiri Au Za Sitta Shawwaal?
Zipi Zinapaswa Kutangulizwa Swiyaam Za Nadhiri Au Za Sitta Shawwaal?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
"Linalokupasa kwanza ni kufunga Swiyaam zilobakia za nadhiri kisha ndio ufunge Sitta za Shawwaal utakapoweza kwa sababu Swiyaam za Sitta Shawwaal ni mustahabb (Sunnah). Ama Swiyaam za nadhiri ni waajib.
[Mawqi’ Shaykh bin Baaz]