20-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Je, Inafaa Kujumuisha Niyyah Ya Sitta Shawwaal Na Swiyaam Za Jumatatu Na Alkhamiys?
Je, Inafaa Kujumuisha Niyyah Ya Sitta Shawwaal Na Swiyaam Za Jumatatu Na Alkhamiys?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Itakapowafikiana kuwa Swiyaam za Masiku ya Sitta Shawwaal yameangukia Jumatatu na Alkhamiys, basi atapata thawabu mbili kwa niyyah ya Swiyaam za Sitta Shawwaal pamoja na niyyah ya Jumatatu na Alkhamiys kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
“Hakika kusihi kwa ‘amali huzingatiwa na niyyah. Na hakika kila mtu atalipwa kwa kile alichokinuia.”
[Al-Fataawaa (20/18-19)]