30-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kuwatolea Zakaatul-Fitwr Familia Hata Kama Wameshajitolea

 Kuwatolea Zakaatul-Fitwr Familia Hata Kama Wameshajitolea

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Anayeishi nchi za ki-Magharibi anaweza kutoa Zakaatul-Fitwr kwa ajili yake na familia yake ikiwa anajua kuwa wameshajitolea wenyewe?"

 

 

JIBU:

 

Zakaatul-Fitwr ambayo ni swaa’ ya chakula kama mchele, ngano, tende au aina yoyote ya chakula, ni kitu ambacho mtu inampasa atoe kwa ajili yake kama kwani ndivyo inavyowajibika kwa sababu Ibn 'Umar (Radhwiya allaahu 'anhuma) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amefaridhisha Swadaqatul-Fitwr kwa Waislamu, aliye huru na mtumwa, mwanaume na mwanamke, mdogo na mkubwa, na ameamrisha itolewe kabla ya watu kwenda kuswali".

 

Ikiwa watu wa nyumba wameshajilipia, basi hakuna haja tena mtu ambaye yuko mbali na familia yake kuwatolea. Bali ajitolee mwenyewe pekee huko anakoishi na ikiwa wako Waislamu ambao wanastahiki kupewa Zakaah hii. Ikiwa hakuna wanaostahiki basi awakilishe familia yake imtolee katika nchi yake ya asili.

 

[Majmuw' Fataawa Ibn 'Uthaymiyn (18/771)]

 

Share