02-Ruqyah: Suwrah, Aayah Na Mengineyo Yaliyothibiti Kutumia Kwa Ajili Ya Ruqyah
Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah
Ruqya: Suwrah, Aayah Na Mengineyo Yaliyothibiti Kwa Ajili Ya Ruqyah
Japokuwa Suwrah kadhaa zimethibiti kusomwa kwa ajili ya kinga na shifaa kutokana na maradhi, au madhara mengineyo kama kupatwa na jicho baya, sihiri, kukumbwa na majini na mashaytwaan, lakini Qur-aan nzima ni shifaa kwa kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ ۖ
Sema: “Hiyo ni kwa walioamini ni mwongozo na shifaa. [Fusw-swilat :44]
Ama Suwrah na Aayah zilizothibiti ni zifuatazo pamoja na dalili zake:
Suwratul-Faatihah:
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ (رضي الله عنه) قَالَ: كُنَّا فِي مَسِيرٍ لَنَا فَنَزَلْنَا فَجَاءَتْ جَارِيَةٌ فَقَالَتْ: "إِنَّ سَيِّدَ الْحَيِّ سَلِيمٌ وَإِنَّ نَفَرَنَا غَيْبٌ فَهَلْ مِنْكُمْ رَاقٍ؟" فَقَامَ مَعَهَا رَجُلٌ مَا كُنَّا نَأْبُنُهُ بِرُقْيَةٍ، فَرَقَاهُ فَبَرَأَ فَأَمَرَ لَهُ بِثَلاَثِينَ شَاةً وَسَقَانَا لَبَنًا فَلَمَّا رَجَعَ قُلْنَا لَهُ: "أَكُنْتَ تُحْسِنُ رُقْيَةً أَوْ كُنْتَ تَرْقِي؟" قَالَ: "لاَ مَا رَقَيْتُ إلاَّ بِأُمِّ الْكِتَابِ." قُلْنَا: "لاَ تُحْدِثُوا شَيْئًا حَتَّى نَأْتِيَ أَوْ نَسْأَلَ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)." فَلَمَّا قَدِمْنَا الْمَدِينَةَ ذَكَرْنَاهُ لِلنَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ: ((وَمَا كَانَ يُدْرِيهِ أَنَّهَا رُقْيَةٌ؟ اقْسِمُوا وَاضْرِبُوا لِي بِسَهْمٍ)).
Amesimulia Abuu Sa'iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Tulikuwa katika safari tukateremka mahali, akaja kijakazi akasema: Bwana wetu ametafunwa na nge na wanaume wetu hawapo, je, yupo kati yenu tabibu? Akasimama pamoja naye mtu mmoja ambaye hatukudhania kuwa anajua ruqyah (utabibu). Akamtibu kwa ruqyah akapona. Akampa kondoo thelathini na akatupa maziwa tunywe (kama ni malipo). Aliporudi tukamwambia: Je, ulikuwa kweli unajua kutibu kwa ruqyah, au ulikuwa unabahatisha tu? Akasema: Hapana, bali nimemsomea Ummul-Kitaab (Suwrah Al-Faatihah). Tukasema: Tusiseme kitu hadi tumfikie au tumuulize Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Tulipofika Madiynah, tulimwelezea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Alijuaje kuwa (Al-Faatihah) ni ruqyah? Gawaneni na mnitolee sehemu (ya kondoo.” [Al-Bukhaariy]
[Rejea: Kutawassal Kwa Suwratul-Faatihah]
Suwratul-Baqarah:
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((لَا تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ مَقَابِرَ إِنَّ الشَّيْطَانَ يَنْفِرُ مِنَ الْبَيْتِ الَّذِي تُقْرَأُ فِيهِ سُورَةُ الْبَقَرَةِ)) رواه مسلم
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Msifanye nyumba zenu makaburi. Kwa hakika shaytwaan haingii nyumba ambayo husomwa humo Suwratul-Baqarah)).
[At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh] na katika Riwaayah ya Muslim, Hadiyth (780):
((Shaytwaan anakimbia nyumba inayosomwa ndani yake Suwratul-Baqarah)).
Sahl bin Sa’d As-Saa’idiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kila kitu kina kipeo cha kudhibiti (na kuangaza yaliyo chini) na Al-Baqarah ndio kipeo cha Qur-aan. Atakayesoma Al-Baqarah usiku nyumbani kwake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba yake nyusiku tatu. Na atakayesoma mchana ndani ya nyumba yake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba hiyo kwa siku tatu)).
[Atw-Twabaraaniy (6/163), Ibn Hibbaan (2/78) na Ibn Mardawayh, Swahiyh At-Targhiyb (2/314)]
Aayatul-Kursiy:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ وَكَّلَنِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِحِفْظِ زَكَاةِ رَمَضَانَ، فَأَتَانِي آتٍ، فَجَعَلَ يَحْثُو مِنَ الطَّعَامِ، فَأَخَذْتُهُ فَقُلْتُ: لأَرْفَعَنَّكَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم. فَذَكَرَ الْحَدِيثَ فَقَالَ: إِذَا أَوَيْتَ إِلَى فِرَاشِكَ فَاقْرَأْ آيَةَ الْكُرْسِيِّ لَنْ يَزَالَ عَلَيْكَ مِنَ اللَّهِ حَافِظٌ، وَلاَ يَقْرَبُكَ شَيْطَانٌ حَتَّى تُصْبِحَ. فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((صَدَقَكَ وَهْوَ كَذُوبٌ، ذَاكَ شَيْطَانٌ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniwakilisha kuhifadhi Zakaah ya Ramadhwaan (Zakaatul-Fitwr). Akaja mtu akaanza kuteka chakula (cha Zakaah) kwa mikono miwili. Nikamkamata na kumwambia: Nitakupeleka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Kisha Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) akahadithia yote na akaongezea “Huyo (Mwizi) akasema kuniambia: “Utakapoingia kitandani kulala, soma Aayatul-Kursiy kwani mlinzi kutoka kwa Allaah atakulinda, na shaytwaan hatokukaribia mpaka asubuhi.” Hapo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Amekwambia ukweli japokuwa yeye ni muongo, naye (huyo mwizi) ni shaytwaan)) [Al-Bukhaariy]
Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah:
عن أَبِي مَسْعُودٍ الأَنْصَارِيِّ، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((الآيَتَانِ مِنْ آخِرِ سُورَةِ الْبَقَرَةِ مَنْ قَرَأَ بِهِمَا فِي لَيْلَةٍ كَفَتَاهُ))
Abuu Mas‘uwd Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayesoma usiku Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah zitamtosheleza)) Yaani: zinamtosheleza kumkinga na kila baya na lenye kumdhuru. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Suwratul-Ikhlaasw Na Al-Mu’awwidhataan (kinga mbili) na Suwratul-Kaafiruwn:
Kwanza, thawabu za kuisoma Suwratul-Ikhlaasw ni sawa na thawabu za thuluthi ya Qur-aan:
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لأَصْحَابِهِ: ((أَيَعْجِزُ أَحَدُكُمْ أَنْ يَقْرَأَ ثُلُثَ الْقُرْآنِ فِي لَيْلَةٍ؟)) فَشَقَّ ذَلِكَ عَلَيْهِمْ وَقَالُوا: أَيُّنَا يُطِيقُ ذَلِكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ فَقَالَ: ((اللَّهُ الْوَاحِدُ الصَّمَدُ ثُلُثُ الْقُرْآنِ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewaambia Maswahaba wake: ((Je, anaweza mmoja wenu asome thuluthi ya Qur-aan katika usiku mmoja?)) Likawa jambo gumu kwao wakasema: Tuwezeje sisi kufanya hivyo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: ((Allaah, Al-Waahidu (Mmoja Pekee, Asw-Swamadu (Mkusudiwa wa yote) ni thuluthi ya Qur-aan)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]
Kuisoma Suwratul-Kaafiruwn thawabu zake ni kama thawabu za kusoma robo ya Qur-aan:
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم :((قُلْ هو اللَّهُ أحَدٌ تعدلُ ثلثَ القرآنِ. و قُلْ يَا أيُّهَا الْكَافِرُونَ تعدلُ ربعَ القرآنِ))
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Sema: “Yeye ni Allaahu Mmoja Pekee)) [112] ni sawa na thuluthi ya Qur-aan na ((Sema: “Enyi makafiri!)) [109] ni sawa na robo ya Qur-aan)) [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Umar, ameisahihisha Al-Albaaniy Taz. Swahiyh Al-Jaami’ (4405), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (586)]
Pia:
عَنْ مُعَاذِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ خُبَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: خَرَجْنَا فِي لَيْلَةٍ مَطِيرَةٍ وَظُلْمَةٍ شَدِيدَةٍ نَطْلُبُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي لَنَا. قَالَ: فَأَدْرَكْتُهُ فَقَالَ: ((قُلْ)). فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا ثُمَّ قَالَ: ((قُلْ)) فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا. قَالَ: ((قُلْ)) قُلْتُ: مَا أَقُولُ؟ قَالَ: ((قُلْ هوَ اللَّهُ أَحَدٌ... وَالْمُعَوِّذَتَيْنِ حِينَ تُمْسِي وَتُصْبِحُ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ تَكْفِيكَ مِنْ كُلِّ شَيْءٍ)). قَالَ أَبُو عِيسَى وَهَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
Imepokelewa kutoka kwa Mu’aadh bin ‘Abdillaah bin Khubayb (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kutoka kwa baba yake kwamba: “Tulitoka usiku mmoja wa kiza kinene na mvua tukimtafuta Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atuswalishe Swalaah.” Akasema: “Nikakutana naye, kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Sema)). Lakini sikusema kitu. Kisha akasema: ((Sema)). Lakini sikusema kitu. Kisha akasema ((Sema)). Nikasema: “Niseme nini?” Akasema: ((Sema: “Yeye ni Allaahu Mmoja Pekee)) [112] … na Al-Mu’awwidhatayni [Al-Falaq na An-Naas 113-114] unapoingia jioni na unapoamka asubuhi mara tatu zitakutosheleza na kila kitu)) [Hadiyth Hasan Swahiyh, Taz. Swahiyh At-Tirmidhiyy (3575), Swahiyh Abiy Daawuwd (5082)]
Al-Falaq na An-Naas:
عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ قَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((أُنْزِلَ - أَوْ أُنْزِلَتْ - عَلَىَّ آيَاتٌ لَمْ يُرَ مِثْلُهُنَّ قَطُّ الْمُعَوِّذَتَيْنِ))
Imepokelewa kutoka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameniambia: ((Imeteremshwa (au) Nimeteremshiwa Aayaat ambazo hazijapatapo kuonekana kabla, Nazo ni Al-Mu’awwidhatayn)) [Muslim, Baab Fadhwl Qiraat Al-Mu’awwidhatyani]
Pia,
عن أَبِي سعيد الخدري: كان رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم يَتَعَوَّذُ من الجَانِّ، وعَيْنِ الإنسانِ، حتى نَزَلَتِ المعُوذَتَانِ، فلما نَزَلَتَا أَخَذَهُما، وتَرَكَ ما سِوَاهُما.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: ‘Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijikinga kutokana na majini na jicho baya la bin Aadam mpaka zilipoteremshwa Al-Mu’awidhataan. Basi zilipoteremshwa, akazishika kujikingia akaacha isipokuwa hizo mbili.” [At-Tirmidhiy, ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (2058)]
Pia,
عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا أَوَى إِلَى فِرَاشِهِ كُلَّ لَيْلَةٍ جَمَعَ كَفَّيْهِ ثُمَّ نَفَثَ فِيهِمَا فَقَرَأَ فِيهِمَا: ((قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ)) وَ ((قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ)) وَ ((قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ)) ثُمَّ يَمْسَحُ بِهِمَا مَا اسْتَطَاعَ مِنْ جَسَدِهِ يَبْدَأُ بِهِمَا عَلَى رَأْسِهِ وَوَجْهِهِ وَمَا أَقْبَلَ مِنْ جَسَدِهِ يَفْعَلُ ذَلِكَ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ.
Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anapanda kitandani kulala kila siku, alikuwa akikusanya viganja vyake vya mkono kisha akipulizia humo kisha akisoma: ((Sema: “Yeye ni Allaahu Mmoja Pekee)) [112] na ((Sema: “Najikinga na Rabb wa mapambazuko)) [113] na ((Sema: “Najikinga na Rabb wa watu)) [114], kisha hujifutia mwilini anapoweza, akianzia kichwani mwake, usoni na mbele, akifanya hivyo mara tatu)). [Al-Bukhaariy, Muslim]
Pia Muislamu asiache kusoma nyiradi za asubuhi na jioni kwani hizo ni kinga kubwa ya kila madhara na balaa.
Kadhaalika, kusoma nyiradi za kulala na kuamka.
Kadhaalika kusema BismiLLaah kabla ya kula au kunywa, na mtu anapoingia na anapotoka katika nyumba, katika kujamiiana, anapoingia msalani pamoja na du’aa zake na kwa ujumla kabla ya kuanza lolote lile ni vizuri kusema BismiLLaah. Rejea: Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)
na Hiswnul Muumin.
Pia kutia wudhuu:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((يَعْقِدُ الشَّيْطَانُ عَلَى قَافِيَةِ رَأْسِ أَحَدِكُمْ إِذَا هُوَ نَامَ ثَلاَثَ عُقَدٍ، يَضْرِبُ كُلَّ عُقْدَةٍ عَلَيْكَ لَيْلٌ طَوِيلٌ فَارْقُدْ، فَإِنِ اسْتَيْقَظَ فَذَكَرَ اللَّهَ انْحَلَّتْ عُقْدَةٌ، فَإِنْ تَوَضَّأَ انْحَلَّتْ عُقْدَةٌ، فَإِنْ صَلَّى انْحَلَّتْ عُقْدَةٌ فَأَصْبَحَ نَشِيطًا طَيِّبَ النَّفْسِ، وَإِلاَّ أَصْبَحَ خَبِيثَ النَّفْسِ كَسْلاَنَ)).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Anapolala mmoja wenu, shaytwaan hufunga kisogoni mwake vifundo vitatu. Hupiga kila kifundo (kumwambia): Umebakiwa na usiku mrefu, basi lala. Anapoamka akamtaja Allaah, kifundo kimoja hufunguka. Anapotawadha, hufunguka kingine, na anaposwali cha tatu hufunguka. Hapo huwa mchangamfu na mwenye nafsi nzuri, na kama si hivyo, huwa na nafsi mbaya na mvivu)). [Al-Bukhaariy]