05-Ruqyah Dhidi Ya Uhasidi Na Jicho Baya
Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah
Ruqyah Dhidi Ya Uhasidi Na Jicho Baya
Muumini hapaswi kuwa na sifa ya uhasidi kwa dalili kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لَا يَجْتَمِعُ الشُّحُّ وَالْإِيمَانُ فِي قَلْبِ عَبْدٍ أَبَدًا))
وفي رواية أخرى قال: ((وَلا يَجْتَمِعُ فِي جَوْفِ عَبْدٍ مُؤْمِنٍ الإِيمَانُ وَالْحَسَدُ)) سنن النسائي كِتَاب الْجِهَادِ باب فَضْلِ مَنْ عَمِلَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ عَلَى قَدَمِهِ - المحدث الألباني خلاصة حكم المحدث صحيح في صحيح النسائي
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Uchoyo na iymaan haviwi pamoja viwili hivi katika moyo wa mja)) na katika Riwaayah: ((Iymaan na uhasidi haviwi pamoja viwili hivi katika moyo wa mja)) [Sunan An-Nasaaiy 3110 Kitaab Al-Jihaad Baab Fadhwl Man ‘Amila Fiy SabiyliLLaah ‘alaa Qadamihi - na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh An-Nasaaiy]
Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatahadharisha:
عنْ أَنَسُ (رضي الله عنه) أنّ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لاَ تَبَاغَضُوا وَلاَ تَحَاسَدُوا وَلاَ تَدَابَرُوا وَلاَ تَقَاطَعوا وَكُونُوا عِبَادَ اللَّهِ إِخْوَانًا وَلاَ يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أَنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلاَثَةِ أَيَّامٍ)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Msibughudhiane [msichukiane], wala msihusudiane, wala msipeane mgongo, wala msikatane, kuweni ndugu enyi waja wa Allaah, wala haifai kwa Muislamu kumhama nduguye kwa zaidi ya siku tatu [asiseme naye])) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na jicho linaweza kuathiri mtu. Inalopasa kwa Muislamu anapomuona nduguye Muislamu amejaaliwa na neema basi ni kumuombea du’aa nzuri kwani imethibiti katika Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba unapomuombea mwenzako kwa siri Malaika huitikia ”Aamiyn” na hukuombea nawe pia kama hivyo unavyomuombea nduguyo au mwenzako. Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
إِذَا رَأَى أَحَدُكُمْ مِنْ أَخِيهِ أَوْ مِنْ نَفْسِهِ أَوْ مِنْ مَالِهِ مَا يُعْجِبُهُ فَلْيُبَرِّكْهُ فَإِنَّ الْعَيْنَ حَقٌّ
Mmoja wenu akiona kwa ndugu yake au kwake, au mali yake kinachomfurahisha akiombee baraka kwani kijicho ni haki. [Hadiyth ya ‘Aamir bin Rabiy’ah na Sahl bin Hunayf (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) - Ahmad (4/447), Ibn Maajah [3509], Maalik [1697, 1698] na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (1/212) na angalia: Tahqiyq Zaad Al-Ma’aad ya Al-Arnaawuwtw (4/170)]
Useme:
اللّهُـمَّ بارِك عَلَـيه أو اللَّهُمَّ بَارِك عَلَيْكَ
Allaahumma Baarik ’alayh au Allaahumma Baarik ‘alayka
Ee Allaah, Mbariki kwa hicho au Allaah Akubariki kwacho
Du’aa za kinga au tiba ya jicho baya na husda:
كَانَ النَّبِيُّ صلَّى اللّه عَلَيْهِ وسَلَّم يَعُوذُ الْحَسَنْ وَالْحُسَيْن
Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwakinga (wajukuu wake) Al-Hasan na Al-Husayn akisema:
أُعيـذُكُمـا بِكَلِـماتِ اللهِ التّـامَّة مِنْ كُلِّ شَيْـطانٍ وَهـامَّة وَمِنْ كُـلِّ عَـيْنٍ لامَّـة
U’iydhukumaa bikalimaatiLLaahit-ttaammati min kulli shaytwaanin wa haammah, wa min kulli ’aynin laammah
Nawakinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia Awakinge kutokana na kila shaytwaan na uvamizi na kila jicho lenye kudhuru [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) Al-Bukhaariy (4/119) [3371]
Kwa hiyo unapotaja kujikinga mwenyewe useme:
أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّةِ مِنْ كُلِّ شَيْطَانٍ وَهَامَّةٍ وَمِنْ كُلِّ عَيْنٍ لاَمَّةٍ
A’uwdhu bikalimaatiLLaahit-ttaammati min kulli shaytwaanin wa haammah, wa min kulli ’aynin laammah
Na pia unaweza kumsomea ruqyah kwa du’aa zifuatazo mtu aliyepatwa na jicho au uhasidi:
بِاسْمِ اللَّهِ أَرْقِيكَ، مِنْ كُلِّ شَيْءٍ يُؤْذِيكَ، مِنْ شَرِّ كُلِّ نَفْسٍ أَوْ عَيْنِ حَاسِد، اللَّهُ يَشْفِيكَ بِاسْمِ اللَّهِ أَرْقِيكَ
BismiLLaahi arqiyka, min kulli shay-in yu-udhiyka, min sharri kulli nafsin aw ‘aynin haasidin, Allaahu Yashfiyka BismiLLaahi arqiyka
((Kwa Jina la Allaah nakusomea ruqyah, kutokana na kila jambo linalokudhuuru, na kutokana na kila nafsi au jicho la hasidi, Allaah Akupe shifaa, kwa Jina la Allaah, nakusomea ruqyah)) [Muslim]
Jibriyl (’Alayhis-Salaam) alimsomea Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) du’aa ifuatayo pindi alipoumwa:
بِاسْمِ اللَّهِ يُبْرِيكَ وَمِنْ كُلِّ دَاءٍ يَشْفِيكَ وَمِنْ شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ وَشَرِّ كُلِّ ذِي عَيْنٍ
BismiLlaahi Yubriyka, wa min kulli daain Yashfiyka, wa min sharri haasidin idhaa hasad, washarri kulli dhiy ‘aynin
((Kwa Jina la Allaah Akubariki, na kutokana kila ugonjwa Akuponyeshe, na kutokana na kila hasidi anapohusudu na kila shari ya jicho)) [Muslim]
Na bila shaka, kusomwe Suwrah na Aayah zilizothibiti za Ruqyah kama Suwratul-Faatihah, Aayatul-Kursiy, Aayah mbili za mwisho katika Suwratul-Baqrah, Suwratul-Ikhlaasw, Al-Mu’awwidhataan (Al-Falaq na An-Naas) na pia Qur-aan nzima ni shifaa ya kila madhara na magonjwa na masaibu.