10-Ruqya: Kutafuta Shifaa: Poza Ya Maradhi, Sihri (Uchawi) Katika Baadhi Ya Vyakula
Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah
Kutafuta Shifaa - Poza Ya Maradhi, Sihri (Uchawi) Katika Baadhi Ya Vyakula
Vifutavyo ni baadhi ya vyakula katika mwongozo wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) vyenye kusababisha kinga na shifaa ya kila aina ya maradhi ikiwemo sihri (uchawi).
1-Asali:
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَأَوْحَىٰ رَبُّكَ إِلَى النَّحْلِ أَنِ اتَّخِذِي مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا وَمِنَ الشَّجَرِ وَمِمَّا يَعْرِشُونَ ﴿٦٨﴾
68. Na Rabb wako Akamtia ilhamu nyuki kwamba: “Jitengenezee nyumba katika majabali, na katika miti, na katika wanavyojenga.”
ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ فَاسْلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلًا ۚ يَخْرُجُ مِن بُطُونِهَا شَرَابٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ فِيهِ شِفَاءٌ لِّلنَّاسِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿٦٩﴾
69. “Kisha kula katika kila matunda, na fuata njia za Rabb wako zilizofanywa nyepesi (kuzipita). Kinatoka katika matumbo yao kinywaji cha rangi mbali mbali ndani yake mna shifaa (ya magonjwa) kwa watu. Hakika katika hayo, bila shaka ni Aayah (ishara, dalili, zingatio) kwa watu wanaotafakari. [An-Nahl: 68-69]
2-Maji Ya Zamzam:
عن جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ (رضي الله عنه) قال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((مَاءُ زَمْزَمَ لِمَا شُرِبَ لَهُ))
Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Maji ya zamzam kwa jambo linaloombewa wakati wa kunywa)) [Ibn Maajah, Ahmad. Taz, Swahiyh Ibn Maajah (2502), Swahiyh Al-Jaami’ (5502)]. Tanbihi: Ingawa kuna udhaifu katika Hadiyth hii lakini kutokana na Shawaahid imekuwa ni Hasan.
3-Habbat Sawdaa – Haba soda
عَنْ عَائِشَةَ (رضي الله عنها) أَنَّهَا سَمِعَتْ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((إِنَّ هَذِهِ الْحَبَّةَ السَّوْدَاءَ شِفَاءٌ مِنْ كُلِّ دَاءٍ إلاَّ مِنْ السَّام))ِ قُلْتُ وَمَا السَّامُ؟ قَالَ: ((الْمَوْتُ))
Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakika Habbat Sawdaa hii ni shifaa kwa kila maradhi isipokuwa sumu)) Nikasema: Nini sumu? Akasema: ((Mauti)) [Al-Bukhaariy, Muslim, Ibn Maajah, Ahmad]
4-Sannaa Na Sannuwt
Sannaa = Majani ya Sanamaki – yanachemshwa na kunywa kwa ajili ya kuendesha na kusafisha tumbo.
Sannuwt = Ima kotmiri mwitu (dill au parsley) au asali kama alivyosema ibn Maajah katika Kitaab Al-Twibb, Hadiyth (3457)
Wengineo wamesema Sannuwt ni aina ya binzari tamu (fennel), au habbat hamraa (sufa/dill seeds) wengine wamesema ni malai au asali inayopatikana katika mbegu. Na Allaah Anajua zaidi
عن أبي أُبَيِّ بْنَ أُمِّ حَرَامٍ رضي الله عنه قال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: ((عَلَيْكُمْ بِالسَّنَى، وَالسَّنُّوتِ، فَإِنَّ فِيهِمَا شِفَاءً مِنْ كُلِّ دَاءٍ، إِلَّا السَّامَ)) قِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَا السَّامُ؟ قَالَ: ((الْمَوْتُ)) روى ابن ماجة (3457) ، والحاكم (7442) ، والطبراني في "مسند الشاميين" (14) ، وأبو نعيم في "الطب النبوي" (177) " وصححه الألباني في " سلسلة الأحاديث الصحيحة" (7442) .
Imepokelewa kutoka kwa Abiy Ubayy bin Ummi Haraam (Radhwiya Allaahu 'anhu) kasema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Tilieni hima kutumia sannah na sannuwt, kwani hivyo viwili ni shifaa (poza) ya kila maradhi isipokuwa sumu)). Akaulizwa: Nini sumu? Akasema: ((Mauti)) [Ibn Maajah (3457), Al-Haakim (7442), Atw-Twabaraaniy katika Musnad Ash-Shaamiyiyn (14), Abuu Na’iym katika Twibb An-Nabawiy (177) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Silsilatul Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (7442)]
5-Tende:
Kula tende saba asubuhi kabla ya kula chochote ni kinga ya sihri (uchawi)
عن عَامِرُ بْنُ سَعْدٍ عَنْ أَبِيهِ (رضي الله عنهما) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((مَنْ تَصَبَّحَ كُلَّ يَوْمٍ سَبْعَ تَمَرَاتٍ عَجْوَةً لَمْ يَضُرَّهُ فِي ذَلِكَ الْيَوْمِ سُمٌّ وَلاَ سِحْرٌ))
Kutoka kwa ‘Aamir bin Sa’d kutoka kwa baba yake (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeamka kila siku asubuhi [akala] tende saba za ‘ajwah haitomdhuru siku hiyo sumu wala sihri [uchawi])) [Al-Bukhaariy. Katika Riwaayah ya Muslim; Kitaab Al-Ashribah imetaja kuliwa asubuhi mapema kabla ya chochote -
Je, Ni Tende Za ‘Ajwah Pekee Zinazopatikana Faida Hiyo?
‘Ajwah ni aina ya tende zinazopatikana mji wa Madiynah lakini ‘Ulamaa wamekubaliana kwamba aina yoyote ya tende zinafaa kupatikana faida iliyotajwa katika Hadiyth hizo.
Imaam bin Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
“Inatarajiwa kuwa Allaah Atanufaisha kwa aina zote za tende ila tu imenukuliwa kuwa ni za Madiynah kutoka na kufadhilishwa kwa tende zake na umakhsusi wake. Na inatarajiwa kuwa Allaah Atanufaisha kwa tende saba zozote zile zikiliwa asubuhi, na huenda Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametaja ametaja hizo kutokana na fadhila zake makhsusi, na utajo maalum kwa tende za Madiynah, haizuii faida aliyoiashiria Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika aina nyinginezo za tende, na nadhani imekuja katika baadhi ya riwaaya "miongoni mwa tende" bila kufungamanisha."
[Majmuw’ Fataawaa bin Baaz (8/109)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Shaykh wetu Ibn Sa’diy (Rahimahu Allaah) alikuwa akiona kwamba hizo 'ajwah ni kwa kupigia mfano tu wa tende, na kwamba iliyokusudiwa ni tende kwa ujumla.”
[Ash-Sharh Al-Mumti’ (5/123) na Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb]
6-Maziwa:
عَنْ طَارِقِ بْنِ شِهَابٍ الأَحْمَسِيِّ (رضي الله عنه) أَنَّ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)) قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ لَمْ يَضَعْ دَاءً إِلاَّ وَضَعَ لَهُ شِفَاءً, فَعَلَيْكُمْ بِأَلْبَانِ الْبَقَرِ فَإِنَّهَا تَرُمُّ مِنْ كُلِّ الشَّجَرِ))
Kutoka kwa Twaariq bin Shihaab Al-Ahmasiyyi (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah (‘Azza wa Jalla) Hakuteremsha maradhi ila Ameyawekea shifaa, basi juu yenu [kunyweni] maziwa ya ng’ombe kwani hayo yanatokana na kila aina ya miti)) [Swahiyh Al-Jaami’ (1808). (1810)]
7-Talbiynah:
عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها أَنَّهَا كَانَتْ تَأْمُرُ بِالتَّلْبِينِ لِلْمَرِيضِ وَلِلْمَحْزُونِ عَلَى الْهَالِكِ، وَكَانَتْ تَقُولُ: إِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((إِنَّ التَّلْبِينَةَ تُجِمُّ فُؤَادَ الْمَرِيضِ، وَتَذْهَبُ بِبَعْضِ الْحُزْنِ))
Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba alikuwa akiamrisha talbiynah kwa ajili ya mgonjwa na mtu aliyefikwa na huzuni kwa ajili ya kufariki mtu wake. Akawa anasema: “Nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakika talbiynah inamtuliza moyo wa mgonjwa na kuufanya mchangamfu na inaondosha baadhi ya huzuni zake)) [Al-Bukhaariy, Kitaab Atw-Twibb, Baab At-Talbiynah Lil-Mariydhw]
عنْ عَائِشَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهَا كَانَتْ إِذَا مَاتَ الْمَيِّتُ مِنْ أَهْلِهَا فَاجْتَمَعَ لِذَلِكَ النِّسَاءُ، ثُمَّ تَفَرَّقْنَ إِلا أَهْلَهَا وَخَاصَّتَهَا، أَمَرَتْ بِبُرْمَةٍ مِنْ تَلْبِينَةٍ فَطُبِخَتْ، ثُمَّ صُنِعَ ثَرِيدٌ فَصُبَّتْ التَّلْبِينَةُ عَلَيْهَا، ثُمَّ قَالَتْ: كُلْنَ مِنْهَا، فَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يقُول: ((التَّلْبِينَةُ مُجِمَّةٌ لِفُؤَادِ الْمَرِيضِ، تَذ هبُ بِبَعْضِ الْحُزْنِ))
Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah mke wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba alikuwa pale mtu alipofariki katika jamaa zake na wanawake wakakusanyika katika nyumba ya aliyefiwa kisha huondoka isipokuwa jamaa zake na rafiki wa karibu kabisa. Huamrisha ipikwe ‘talbiynah’ (uji wa unga wa shayiri). Kisha ‘thariyd’ (mikate katika supu ya nyama) hupikwa na ‘talbiynah’ humiminwa juu yake. Kisha ‘Aaishah huwaambia wanawake: “Kuleni kwani nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Talbiynah inapooza moyo wa mgonjwa na inaondosha baadhi ya huzuni.” [Al-Bukhaariy katika Kitaab Atw-Twa’aam, Muslim katika Baab As-Salaam]
عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها قَالَتْ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((عَلَيْكُمْ بِالْبَغِيضِ النَّافِعِ التَّلْبِينَةِ)). يَعْنِي الْحَسَاءَ. قَالَتْ وَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا اشْتَكَى أَحَدٌ مِنْ أَهْلِهِ لَمْ تَزَلِ الْبُرْمَةُ عَلَى النَّارِ حَتَّى يَنْتَهِيَ أَحَدُ طَرَفَيْهِ . يَعْنِي يَبْرَأُ أَوْ يَمُوتُ .
Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kuleni faida ya talbiynah inayochukizwa [asiyeipenda mgonjwa])) Yaani uji wa shayiri. Akasema: “Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa pindi anapolalamika mtu katika ahli yake, basi sufuria ya kupikia haindokani katika moto mpaka mawili yatokee.” Yaani: ima apone mtu huyo au afariki. [Swahiyh Sunan Ibn Maajah 3446)]
عَنْ عَائِشَة رضي الله عنها عن النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((عليكم بالبغيضِ النافعِ التلبينةِ والذي نفسي بيده إنها لتغسل بطن أحدكم كما يغسل أحدكم الوسخ عن وجهه بالما))
Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kuleni kitu chenye faida ambacho hakipendwi kuliwa (na mgonjwa); talbiynah. Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, hakika hiyo inasafisha tumbo la mmoja wenu kama anavyosafisha mmoja wenu uchafu wa usoni mwake kwa maji)) [Sunan An-Nasaaiy Al-Kubraa (7575) na Mustadrak ‘Alaa Asw-Swahiyhayn]
Anaweza pia mtu kutumia dawa za asilia zinazojulikana kuponyesha maradhi mfano kutokana na mitishamba, mbegu n.k. ambazo zimetajwa katika kitabu cha Twibbun-Nabawiy (Tiba ya Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) cha Imaam Ibnul-Qayyim (Rahimahu-Allaah) na ‘Ulamaa wengineo.
Tiba Makhsusi Ya Sihri (Uchawi) Kwa Kutumia Majani Ya Mkunazi:
a-Unaweza kufuata njii hii ya Imaam Ibn Hajar:
Amesema Al-Hafidhw bin Hajar (Rahimahu Allaah): (Mtu) Achukue majani saba ya Sidri (Kunazi) (yaliyo) mabichi kisha ayatwange kati ya mawe mawili, kisha ayachanganye na maji na (kisha) ayasomee Ayatul-Kursiyy na Al-Qawaaqil: (Suwrah Al-Jinn, Al-Kaafiruwn, Al-Ikhlaasw, Al-Falaq, An-Naas) kisha avivie (apulizie) mara tatu na kisha ayaoge, basi, itamuondoshea yote yaliyomsibu. Na ni nzuri pia kwa yule aliyezuiwa (ashindwaye kumuingilia) Ahli yake kwa uchawi." [Fat-hul Baariy (10/233)]
Al-Qawaaqil ni Suwrah zinazoanzia na قُلْ nazo ni: Al-Jinn (72), Al-Kaafiruwn (109), Al-Ikhlaasw (112), Al-Falaq (113), An-Naas (114)
b-Na juu ya hivyo somea Suwrah na Aayah zifuatazo:
Al-Faatihah
Aayatul-Kursiyy
Aayah mbili za mwisho wa Suwrah Al-Baqarah
Aayah namba 117 - 122 Suwrah Al-A'raaf (7)
Aayah namba 79 - 82 Suwrah Yuwnus (10)
Aayah namba 65 - 70 Suwrah Twaahaa (20)
Adhkaar nyenginezo za kinga na du'aa za kuomba Shifaa na kwa ujumla Qur-aan kwa wingi.
Pia, kufanya hijaamah (kuumikwa au kupigwa chuku)
[Al-'Ilaaj Bir-Ruqaa Minal-Kitaabi Was-Sunnah - Sa'iyd Bin 'Aliy Bin Wahf Al-Qahtwaaniy]
Mkunazi Mawe Mawili