Imaam Al-Albaaniy: Haikuthibiti Kuwa Malaika Anayetoa Roho Anaitwa Izraaiyl
Haikuthibiti Kuwa Malaika Anayetoa Roho Anaitwa Izraaiyl
Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, ni sahihi kusema jina la Malaika anayetoa roho kuwa anaitwa Izraaiyl?
JIBU:
Hakuna chochote kilicho sahihi kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kumwita Malaika anayetoa roho kuwa ni Izraaiyl.
[Fataawaa Imaam Al-Albaaniy – Madiynah Wal-Imaaraat]
Tanbihi:
Lilothibiti katika Qur-aan ni kwamba Malaika anayetoa roho ametajwa kama ni Malakul-Mawt (Malaika wa kutoa roho) katika kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
قُلْ يَتَوَفَّاكُم مَّلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ ﴿١١﴾
“Atakufisheni Malaika wa mauti ambaye amewakilishwa kwenu, kisha kwa Rabb wenu mtarejeshwa.” [As-Sajdah: 11]
Lakini haimaanishi kuwa ndio jina lake bali ametajwa hivyo kama ni sifa ya kitendo hicho cha kutoa roho.
Na Allaah Anajua zaidi