Shaykh Fawzaan: Kuamiliana Na Watu Wa Bid’ah

 

Kuamiliana Na Watu Wa Bid’ah

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Amesema Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah):

 

“Inaharamishwa kufanya ziara kwa Mubtadi’ (Mzushi) na kukaa naye isipokuwa tu kwa upande wa nasiha na kumkataza au kumuonya (uzushi) alionao. Kwa sababu kuchanganyika naye ni shari, na kunaeneza uadui kwa wengine. Kadhalika inapasa kuwahadharisha, na kutahadharisha shari zao.

 

“Kama ambavyo, haiwezekani kuchukua (elimu) kutoka kwao. Na (inapaswa) kuwazuia wasifanye bid’ah, na isipowezekana (kuwazuia) basi itapasa ‘Ulamaa Waislamu na Viongozi kuwazuia bid’ah (zao) na kuzuia watu wasichukue (elimu) kwa hao watu wa bid’ah, na kuwarudi kwa hoja shari zao; kwani khatari yao kwa Uislamu ni mkubwa.”

 

 

[‘Aqiydatu At-Tawhiyd, uk. 199]

 

 

Share