02-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Iko Daraja Ya Juu Kabisa
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah
02-Laa Ilaaha Illa Allaah: Iko Daraja Ya Juu Kabisa
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((الإيمَانُ بِضْعٌ وَسَبْعُونَ)) أَوْ ((بِضْعٌ وَسِتُّونَ شُعْبَةً، فَأَفْضَلُهَا قَوْلُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الأَذَى عَنْ الطَّرِيقِ، وَالْحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنْ الإِيمَانِ)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Iymaan ni sabiini na kitu)) au alisema ((Tanzu sitiini na kitu. Ilio bora kabisa ni kauli ya ‘Laa ilaaha illa-Allaah’, na ya chini kabisa ni kuondosha taka njiani. Na kuona hayaa ni utanzu katika tanzu za Iymaan)). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Faida: Bidhw’ ni idadi baina ya tatu na tisa.