Shaykh Fawzaan: Maana Ya Ikhlaasw Katika ‘Amali
Maana Ya Ikhlaasw Katika ‘Amali
Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Nini maana ya ikhlaasw? Na nini hukmu yake ikiwa mja atakusudia kinginecho (asiyekuwa Allaah) je, nini hukmu yake?
JIBU:
Maana ya ikhlaasw ni kusalimika na shirki na kitendo cha mja kiwe kimekusudiwa na kutiliwa niyyah safi kwa ajili ya kutafuta Wajihi wa Allaah (‘Azza wa Jalla), kusiweko na shirki humo wala riyaa (kujionyesha) wala kutafuta umaarufu, wala kisikusudiwe asiyekuwa Allaah (‘Azza wa Jalla), wala asitake mtu humo (manufaa ya) dunia, au kusifiwa na watu.
Bali iwe 'amali ni ya kumsafishia niyyah Allaah (‘Azza wa Jalla) kwa sababu Allaah Hapokei ‘amali isipokuwa ziwe zenye kumsafishia niyyah yeye Subhaanahu wa Ta’aalaa.”