Imaam Ash-Shaatwibiy: Bid’ah Itakapokithiri, Wajinga Wataona Ni Jambo La Haki
Bid’ah Itakapokithiri, Wajinga Wataona Ni Jambo La Haki
Imaam Ash-Shaatwiby (Rahimahu Allaah)
Amesema Imaam Ash-Shaatwiby (Rahimahu Allaah):
“Bid’ah na mikhalafaat itakapokithiri na watu wakashirikiana juu ya hayo (maovu), basi (itafikia wakati) mjinga (ataona bid'ah ndio Sunnah) atasema: “Kama ungekuwa huu ni munkar (ovu) basi wasingefanya watu.”
[Al-I’tiswaam (2/271)]
