Shaykh Fawzaan: Qadhiya Zenye Mmuliko Na Muhimu Ambazo Waislamu Wanakabiliana Nazo Katika Zama Hizi
Qadhiya Zenye Mmuliko Na Muhimu Ambazo Waislamu Wanakabiliana Nazo Katika Zama Hizi
Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Ni zipi qadhiya zenye mmuliko na muhimu ambazo zinahitaji kisimamo cha Waislamu (kupambana nazo) katika zama hizi?
JIBU:
Qadhiya zenye mmuliko na muhimu ambazo zinahitaji kisimamo cha Waislamu (kupambana nazo) katika zama hizi ni qadhiya ya ujinga katika ‘Aqiydah ya Tawhiyd (ambalo lipo) kwa wengi wanaojinasibisha na Uislamu, na (pia qadhiya) za wale wanaojiegemeza kwenye madhehebu yenye kwenda kinyume na Uislamu, na (pia qadhiya) za uvamizi wa kifikra wa Kikafiri ulioingia kutoka nchi za Kikafiri kuingia katika nchi za Kiislamu.
Qadhia zote hizi zinahitajia mmuliko na msimamo sahihi na kupingwa kwa nguvu na hilo (linahitajia kukabiliwa) kwa kuubainisha Uislamu kwa 'Aqiydah yake iliyo sahihi na shariy'ah zake zenye hekima. Na kutahadharisha kila linalokwenda kinyume nao (Uislamu) kupitia Manhaj za mafunzo na njia za vyombo vya khabari na kwa kueneza vitabu vyenye manufaa.
[Al-Muntaqa Min Fataawaa Ash-Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (1/416)]