Imaam Maalik: ‘Ilmu (Elimu) Isichukuliwe Kutoka Kwa Aina Nne Za Watu
‘Ilmu (Elimu) Isichukuliwe Kutoka Kwa Aina Nne Za Watu
Imaam Maalik (Rahimahu Allaah)
Amesema Imaam Maalik (Rahimahu Allaah):
“Ilmu isichukuliwe kutoka kwa watu wa aina nne:
Mjinga anayefanya ujinga wake hadharani, hata kama amesimulia riwaya nyingi;
Na Mzushi anayelingania katika matamanio yake;
Na mtu anapoongea na watu husema uongo, hata kama simtuhumu kusema uongo katika Hadiyth;
Na mja mwema mfanya 'ibaadah sana ambaye hakumbuki (haihifadhi) anachokisimulia (katika Hadiyth)."
[Siyar A’laam An-Nubalaa (7/163)]