175-Asbaabun-Nuzuwl: Al-A'raaf Aayah 175: وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-A’raaf 175
175-Na wasomee (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) khabari za yule Tuliyempa Aayaat (ishara, dalili) Zetu, akajivua nazo na shaytwaan akamfuata, na akawa miongoni mwa waliopotoka.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ ﴿١٧٥﴾
Na wasomee (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) khabari za yule Tuliyempa Aayaat (ishara, dalili) Zetu, akajivua nazo na shaytwaan akamfuata, na akawa miongoni mwa waliopotoka.
وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا وَلَـٰكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الْأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ ۚ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ الْكَلْبِ إِن تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَث ۚ ذَّٰلِكَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ فَاقْصُصِ الْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ ﴿١٧٦﴾
Na lau Tungelitaka Tungelimnyanyua kwazo (hizo Aayaat), lakini aligandamana na dunia na akafuata hawaa zake. Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa, ukimhujumu ananing’iniza ulimi nje na kuhema, na ukimwacha pia ananing’iniza ulimi nje na kuhema. Hivyo ndiyo mfano wa watu waliokadhibisha Aayaat Zetu. Basi simulia visa huenda wakatafakari.
سَاءَ مَثَلًا الْقَوْمُ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَأَنفُسَهُمْ كَانُوا يَظْلِمُونَ ﴿١٧٧﴾
Uovu ulioje mfano wa watu waliokadhibisha Aayaat Zetu na wakawa wanajidhulumu nafsi zao! [Al-A’raaf (7:175-177)]
Sababun-Nuzuwl:
Mja Aliyepewa Siri Ya Jina Tukufu Kabisa La Allaah (سبحانه وتعالى) Lakini Alifuata Shaytwaan Akapotoka.
Aayah hii na zinazofuatia (7:175-177) zimeteremshwa kuhusu kisa cha Bal’aam ibn Baa’uwraa katika kizazi cha Bani Israaiyl. Alijaaliwa kuwa na ‘Ilmu ya hali ya juu na akajulishwa Jina t Tukufu kabisa la Allaah (سبحانه وتعالى). Lakini akapotoka kwa sababu ya kufuata matamanio na anasa za dunia. Baada ya kushawishiwa na waovu, alikubali kuomba Du’aa dhidi ya Nabiy Muwsaa (عليه السلام) kwa ajili ya kuchuma maslahi ya kidunia. Riwaaya nyengine inasema zimeteremka kumhusu Umayyah bin Abi Asw-Swalt. Riwaayah nyingine ni mtu kutoka Yemen aliyeitwa Bal’am. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]