012-Aayah Na Mafunzo: Rahma Za Allaah Zinashinda Ghadhabu Zake
Aayah Na Mafunzo
Al-An’aam 12
012-Rahma Za Allaah Zinashinda Ghadhabu Zake
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
قُل لِّمَن مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ قُل لِّلَّـهِ ۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٢﴾
Sema: Ni vya nani vilivyomo mbinguni na ardhini? Sema: Ni vya Allaah. Amejiwajibishia Nafsi Yake Rahmah. Bila shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah, hapana shaka yoyote ndani yake. Wale ambao wamekhasiri nafsi zao basi wao hawaamini. [Al-An'aam: 12]
Mafunzo:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: (( لَمَّا قَضَى اللَّهُ الْخَلْقَ كَتَبَ فِي كِتَابِهِ عَلَى نَفْسِهِ فَهُوَ مَوْضُوعٌ عِنْدَهُ إِنَّ رَحْمَتِي تَغْلِبُ غَضَبِي)) البخاري مسلم النسائي وابن ماجه
Kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Allaah Alipoumba viumbe Aliandika katika kitabu Chake Alichonacho katika Nafsi Yake: Rahmah Zangu zinashinda ghadhabu Zangu)) [Al-Bukhaariy, Muslim, an-Nasaaiy na Ibn Maajah]