19-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Maneno Bora Kabisa Waliyotamka Manabii Wote
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah
19-Maneno Bora Kabisa Waliyotamka Manabii Wote
عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما أن النَّبِيّ صلى الله عليه وسلم قال: ((خَيْرُ الدُّعَاءِ دُعَاءُ يَوْمِ عَرَفَةَ، وخَيْرُ مَا قُلْتُ أنَا وَالنَّبيُّونَ مِنْ قَبْـلِي: لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ قَدِير)) روى الترمذي
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya 'Arafah, na yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Manabii kabla yangu ni: “Laa Ilaaha illa Allaah Wah-dahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr” [Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Hana mshirika, ufalme wote ni Wake, na Himdi zote ni Zake, Naye ni Mweza wa kila kitu])) [Swahiyh At-Tirmidhiy (3/184), Silsilatu Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (4/6), Swahiyh At-Targhiyb (1536)]