Swalah Inavyoswaliwa Wakati Uko Safarini
SWALI:
ASSALAAMU ALAYKUM NDUGU ZANGU,
ALHAMDULILLAH TANGU KUPATA KWA REHEMA YA ALLAH(S.W,T.) HII WEB SITE NIMEFADIKA SANA NA NIMEPATA MAJIBU YA MASWALA MENGI YALIYYO KUWA YAKINI HANGAISHA.NIME SOMA HABARI YA SWALAH YA SAFARI LAKINI KUNA SWALA MOJA AMBAYO SIKU PATA MAJIBU NDANI YA TEXT HIYO.
SWALI NI: JEE IKIWA TUNASAFIRI KUTOKA
JAZAAKALLAHUKHEIR BAARAKALLAHU FIIHI FIAMANILLAH
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukran kwa swali lako zuri na muhimu
Mbali na yote hayo ifahamike kuwa hakuna udhuru wa kuacha Swalah. Mtu anaweza kuchelewa kwa sababu zinazokubalika katika sheria, nazo ni kusahau, kulala, kujumuisha baina ya walah mbili mtu akiwa katika safari, kutotambua kuwa wakati wa Swalah umeingia mpaka ukatoka na kadhalika.
Jambo la muhimu la kufanya kwa sababu wewe uko katika safari hufai kuacha Swalah ikakupita. Allah Aliyetukuka Ametuonea huruma tukiwa katika hali hiyo kuwa tunaweza kuswali Swalah ya safari na kupunguza. Kwa mfano umeingia katika ndege na ipo angani, zipo ndege nyingine ambazo wametenga sehemu za kuswalia, hivyo wakati ukifika mtaswali ndani. Ikiwa hakuna sehemu iliyotengwa basi utajaribu kutafuta Qiblah na kuelekea pale ambapo una yakini kuwa ndipo sehemu ya Qiblah. Katika hali hiyo utaswali kwa kuketi. Ndege zinazomilikiwa na nchi za Kiislamu aghlabu
Mfano umetoka asubuhi na Swalah ya Adhuhuri imekukuta ukiwa angani na pengine pia Swalah ya Alasiri, hivyo unaweza kuchagua kuswali ima Swalah zote mbili wakati wa Adhuhuri au zote mbili wakati wa Alasiri. Utakavyoswali katika nyakati hizo mbili, utaswali rakaa mbili kisha utatoa salamu na kuswali nyingine mbili. Na Swalah ya Maghrib na ‘Ishaa pia unazichanganya lakini Swalah ya Maghrib utaswali vile vile rakaa tatu bila kupunguza na ya ‘Ishaa utaswali mbili.
Kwa manufaa na maelezo zaidi bonyeza kiungo kifuatacho:
Na Allah Anajua zaidi