Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Ramadhwaan: Hukmu Ya Aliyefariki Akiwa Ana Deni La Swiyaam Za Ramadhwaan

 

Hukmu Ya Aliyefariki Akiwa Ana Deni La Swiyaam Za Ramadhwaan

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya mtu aliyefariki na huku anadaiwa Swiyaam za Ramadhwaan? 

 

 

JIBU:

 

Ikiwa amefariki na huku anadaiwa Swiyaam za Ramadhwaan, basi mmoja wa  aliyekuwa na jukumu la mambo yake katika jamaa zake walio karibu naye au warithi wake wafunge kwa ajili yake. Hii imetajwa katika Hadiyth kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Yeyote aliyekufa wakati ana deni la (Swawm) ya Ramadhwaan, basi yule mwenye jukumu la mambo yake afunge kwa ajili yake)).

 

Ikiwa aliyekuwa na jukumu la mambo yake hatofunga kwa ajili yake basi amlishe masikini mmoja kwa kila siku moja aliyokuwa akidaiwa.

 

 

[Imaam  Ibn ‘Uthyamiiyn Fataawa Ramadhwaan - Mjalada 2, Ukurasa 626, Fatwa Namba 626; Fiqh Al-'Ibaadaat libni 'Uthaymiyn - Ukurasa 202-203]

 

Share