24-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah… Allaah Humsadiki Na Akiwa Katika Ugonjwa Akafa Ameahidi Kuwa Moto Hautamla.
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah
24-Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah, Wa-Allaahu Akbar....
Allaah Humsadiki Na Akiwa Katika Ugonjwa Akafa Ameahidi Kuwa Moto Hautamla.
عن أَبي سعيد الخُدْرِيِّ وأَبي هريرة رضيَ اللَّه عنهما ، أَنهُما شَهِدَا على رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَنه قال: ((مَنْ قَالَ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ ، صَدَّقَهُ رَبُّهُ فَقَالَ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَأَنَا أَكْبَرُ ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ ، قَالَ اللَّهُ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَحْدِي ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ ، قَالَ اللَّهُ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَحْدِي لا شَرِيكَ لِي ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ ، قَالَ اللَّهُ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا لِيَ الْمُلْكُ وَلِيَ الْحَمْدُ ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَلا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلا بِاللَّهِ ، قَالَ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَلا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلا بِي)) وَكَانَ يَقُولُ: ((مَنْ قَالَهَا فِي مَرَضِهِ ثُمَّ مَاتَ لَمْ تَطْعَمْهُ النَّارُ))
Abu Sa’iyd Al-Khudriyy na Abu Hurayrah (رضي الله عنهما), wameshuhudia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayesema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa”, Rabb wake Amemsadiki, Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, Nami ni Mkubwa”. Na akisema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake”. Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, Peke Yangu”. Na akisema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Mpweke Hana mshirika”, Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi Peke Yangu Sina mshirika”. Na akisema; “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, ni Wake Ufalme na Himdi ni Zake”, Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, Ufalme ni Wangu na Himdi ni Zangu”. Na Akisema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah na hapana uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Allaah”. Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi na hapana uwezo wala nguvu isipokuwa Zangu.”)) Na Alikuwa (Nabiy (صلى الله عليه وسلم) akisema: ((Atakayesema hayo akiwa mgonjwa akafariki, moto hautamla)) [At-Tirmidhiy [3430], Ibn Maajah [3794], na ameisahihisha Al-Albaaniy. Taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/152), Swahiyh Ibn Maajah (2/317), Swahiyh At-Targhiyb (3481)]