02-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Hujaji Kubakia Majumbani Wiki Wanaporudi Kwao Bila Kwenda Swalaah Ya Jamaa
Hujaji Kubakia Majumbani Wiki Wanaporudi Kwao Bila Kwenda Swalaah Ya Jamaa
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Baadhi ya Hujaji wanaporudi kwao kutoka ardhi tukufu (Makkah) hubakia majumbani mwao muda wa wiki hawatoki nje, hata inapombidi atoke, wala hawaendi Msikitini kuswali, wanabaki kupokea watu ili wawaombee du'aa. Je hivi ni Sunnah?
JIBU:
Haikuthibitika katika Sunnah, bali ni bid’ah na ni makosa kwa yeyote anayeamini kuwa ni Sunnah.
Kubakia majumbani na kukosa kuhudhuria Swalaah ya Jamaa Misikitini hairuhusiwi isipokuwa kwa sababu zilizokubalika katika katika Shariy’ah. Kwa hiyo kuacha kuhudhuria Swalaah ya Jamaa ni dhambi.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Al-Bid'ah wal-Muhdathaat Wa Maa Laa Aswala Lahu – Uk. 406]