02-Imaam Ibn Baaz: Wudhuu Katika Twawaaf Na Sa’ay

 

Wudhuu Katika Twawaaf Na Sa’ay

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, ni lazima kuwa na wudhuu ili kufanya twawaaf na sa’ay?

 

JIBU:

 

Kuwa na wudhuu ni lazima kwa ajili ya twawaaf pekee. Ama sa’ay ni bora kuwa na wudhuu. Lakini pindi ukimtoka mtu wudhuu basi sa’ay hubakia kuwa ni sahihi.

 

[Fataawa al-Hajj wal ‘Umrah waz-Ziyaarah]

 

 

Rai Za ‘Ulamaa Wengineo Kuhusu Kulazimika Wudhuu Katika Twawaaf:

 

Rai za ‘Ulamaa wengineo kama Imaam Ibn Haniyfah (Rahimahu Allaah), Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) katika Majmuw’ Al-Fataawaa (21/273),  wameona kwamba wudhuu haulazimiki katika Twawaaf.  Pia Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) ambaye ametoea maelezo marefu kuhusiana na swala hili katika Ash-Sharh Al-Mumti’ (7/300), kwamba hakuna ulazima wa kuwa na wudhuu katika twawaaf.   Akataja pia mashaka ya kutoka nje ya twawaaf kwenda kutafuta sehemu za kutia wudhuu kwa zama hizi ambazo ni zahma kubwa mno humo Masjid Al-Haraam, khasa katika twawaaf. Hivyo akafutu kuwa mtu akitokwa na pumzi na wudhuu wake ukharibika basi aendelee tu kutekeleza twawaaf yake bila ya kwenda kutia wudhuu kwa ajili ya kuendeleza au  kuanza upya, na twawaaf yake itakuwa Swahiyh In Shaa Allaah.

 

 

Share