04-Imaam Ibn Baaz:Twawaaf Na Sa’y Wakati Swalaah Ya Fardh Inaanza
Twawaaf Na Sa’y Wakati Swalaah Ya Fardh Inaanza
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya kutokumaliza twawaaf au Sa’y wakati Swalaah ya fardh imeanza kuswaliwa?
JIBU:
Inampasa asite, na aswali katika Jamaa, kisha aendelee twawaaf na sa’y yake pale alipofikia kabla ya kuanza Swalaah.
[Fataawa al-Hajj wal-‘Umrah waz-Ziyaarah – uk. 80]