06-Imaam Ibn Baaz: Kulazimika Kuswali Rakaa Mbili Nyuma Ya Maqaam Ibraahiym
Kulazimika Kuswali Rakaa Mbili Nyuma Ya Maqaam Ibraahiym
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, ni lazima kuswali Rakaa mbili baada ya kumaliza twawaaf nyuma ya Maqaam Ibraahiym? Nini hukmu ya mwenye kusahau kuziswali?
JIBU:
Sio lazima kuswali Rakaa mbili nyuma ya Maqaam Ibraahiym, bali inakuwa ni sahihi hata akiswali mtu popote kwengine katika Masjidul-Haraam. Vile vile hakuna madhara kwa anayesahau kuziswali kwani hizo ni Sunnah na sio fardhi.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawa al-Hajj wal-'Umrah waz-Ziyaarah uk. 81]