10-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Amefanya Twawaaful-Widaa'i Kisha Hakuweza Kuondoka Makkah Wakati Huo
Amefanya Twawaaful-Widaa'i Kisha Hakuweza Kuondoka Makkah Wakati Huo
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Mtu amefanya Hajj, alipomaliza kafanya twawaaful-widaa'i usiku lakini akashindwa kuondoka Makkah baada ya twawaaf, hivyo akabakia Makkah hadi asubuhi kisha akasafiri. Nini hukmu ya yake?
JIBU:
Shariy’ah inavyopasa ni kuwa twawaaful-widaa'i iwe pindi mtu anapokuwa tayari kuondoka Makkah pale pale kutokana na Hadiyth kutoka kwa Ibn 'Abbaas: "Watu waliamrishwa kuwa kitendo chao cha mwisho (kabla ya kuondoka Makkah) kiwe ni twawaaf katika Ka'abah, isipokuwa kwa wanawake wenye hedhi". [Al-Bukhaariy na Muslim].
Hivyo ikiwa alifanya twawaaf kwa niyyah ya kuondoka usiku kisha akazuilika hadi asubuhi, basi hakuna ubaya In Shaa Allaah. Akiweza kurudia twawaaful-widaa'i kabla ya kuondoka ni bora zaidi.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawa al-Hajj wal-'Umrah waz-Ziyaarah – Uk.84]