10-Wasiya Kumi Katika Mwisho Wa Suwrah Al-An'aam: Kufuata Njia Iliyonyooka Na Sio Njia Nyinginezo
Wasiya Kumi Katika Mwisho Wa Suwrah Al-An'aam
10- Kufuata Njia Iliyonyooka Na Sio Njia Nyinginezo
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ﴿١٥٣﴾
“Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa.” [Al-An’aam: 153]
Wasiya huu wa kumi ni muhimu kabisa kutekelezwa kwa sababu ni njia ya Muislamu kijiweka katika usalama wa Dini yake kwa kubakia katika Tawhiyd, Dini safi na kuthibitisha iymaan na taqwa yake na pia ujieupusha na shari za shaytwaan. Kubakia katika Njia iliyonyooka ni kubakia katika nyendo za Salafus-Swaalih (Wema waliopita).
Ufafanuzi wa Swiraatwul-Mustaqiym (Njia iliyonyooka) kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
عَنْ جَابِر قَالَ : "كُنَّا جُلُوسًا عِنْد النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَخَطَّ خَطًّا هَكَذَا أَمَامه فَقَالَ ((هَذَا سَبِيل اللَّه)) وَخَطَّيْنِ عَنْ يَمِينه وَخَطَّيْنِ عَنْ شِمَاله وَقَالَ ((هَذِهِ سُبُل الشَّيْطَان)) ثُمَّ وَضَعَ يَده فِي الْخَطّ الْأَوْسَط ثُمَّ تَلَا هَذِهِ الْآيَة" ((وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُل فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَنْ سَبِيله ذَلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ)) وَرَوَاهُ أَحْمَد وَابْن مَاجَهْ
Kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: “Tulikuwa tumekaa pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akachora mstari mbele yake, akasema: ((Hii ni njia ya Allaah)). Kisha akachora mistari miwili upande wa kulia (wa huo mstari mkuu) na miwili upande wa kushoto yake, kisha akasema: ((Hizi njia za shaytwaan)) Kisha akaweka mkono wake katika njia ya katikati akasoma:
وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُل فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَنْ سَبِيله ذَلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
((Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa.”)) [Ahmad na Ibn Maajah]
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametoa maonyo mengi na kutahadharisha tusitoke nje ya Swiraatwul-Mustaqiym (Njia iliyonyooka), akafafanua katika Hadiyth:
عَنْ النَّوَّاس بْن سَمْعَان عَنْ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((ضَرَبَ اللَّه مَثَلًا صِرَاطًا مُسْتَقِيمًا وَعَنْ جَنْبَيْ الصِّرَاط سُورَانِ فِيهِمَا أَبْوَاب مُفَتَّحَة وَعَلَى الْأَبْوَاب سُتُور مُرْخَاة وَعَلَى بَاب الصِّرَاط دَاعٍ يَقُول يَا أَيّهَا النَّاس اُدْخُلُوا الصِّرَاط الْمُسْتَقِيم جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا وَدَاع يَدْعُو مِنْ فَوْق الصِّرَاط فَإِذَا أَرَادَ الْإِنْسَان أَنْ يَفْتَح شَيْئًا مِنْ تِلْكَ الْأَبْوَاب قَالَ وَيْحك لَا تَفْتَحهُ فَإِنَّك إِنْ تَفْتَحهُ تَلِجهُ فَالصِّرَاط الْإِسْلَام وَالسُّورَانِ حُدُود اللَّه وَالْأَبْوَاب الْمُفَتَّحَة مَحَارِم اللَّه وَذَلِكَ الدَّاعِي عَلَى رَأْس الصِّرَاط كِتَاب اللَّه وَالدَّاعِي مِنْ فَوْق الصِّرَاط وَاعِظ اللَّه فِي قَلْب كُلّ مُسْلِم)) وَرَوَاهُ التِّرْمِذِيّ وَالنَّسَائِيّ
Kutoka kwa An-Nawwaas bin Sam’aan kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Ametoa mfano wa Swiratwul-Mustaqiym [njia iliyonyooka] na katika pande mbili za hii njia, kuna kuta mbili zilizokuwa na milango ya kutokea. Katika milango hiyo, kuna mapazia yaliyoteremshwa chini. Na katika mlango wa njia hii kuna muitaji “Enyi watu! Njooni muingie katika Njia Iliyonyooka pamoja msigawanyike”. Kisha kuna muitaji mwengine anayeita kutoka juu ya njia ambaye humwambia mtu anapotaka kuondosha pazia katika milango yoyote hii. “Ole wako! Usifungue mlango huu, kwani ukiufungua utakuja kuingia humo. Njia Iliyonyooka ni Uislamu. Kuta mbili ni mipaka ya Allaah. Milango iliyofunguliwa inaongoza katika maharimisho ya Allaah. Muitaji katika lango la njia ni kitabu cha Allaah (Qur-aan), na muitaji kutoka juu ya njia ni mawaidha ya Allaah katika moyo wa kila Muislamu)) [Ahmad]
Na akasisitiza kubakia katika manhaj yake ili Muislamu abakie salama katika Dini yake. Miongoni mwa matahadharisho yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na masisitizo hayo ni Hadiyth zifuatazo:
Amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
((افترقت اليهود على إحدى وسبعين فرقة، وافترقت النصارى على اثنتين وسبعين فرقة، وستفترق هذه الأمة على ثلاث وسبعين فرقة كلها في النار إلا واحدة)) فقال الصحابة: من هي يا رسول الله؟ قال: ((من كان على مثل ما أنا عليه وأصحابي)) الترمذي والحاكم
((Waligawanyika Mayahudi katika makundi sabini na moja, na waligawanyika Manaswara katika makundi sabini na mbili, na utagawanyika Umma wangu katika makundi sabini na tatu, yote yataingia motoni ila moja!)) Maswahaba wakasema: 'Ni kundi lipi hilo Ee Rasuli wa Allaah? Akajibu: ((Ni lile ambalo litakuwa katika mwenendo wangu hii leo na Maswahaba zangu)) [Imepokewa na Maimaam At-Tirmidhiy na Al-Haakim]
Na akasema pia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
((أُوصِيكُمْ بِتَقْوى اللَّه، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وإِنْ تَأَمَّر عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حبشيٌ، وَأَنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيرى اخْتِلافاً كثِيرا. فَعَلَيْكُمْ بسُنَّتي وَسُنَّةِ الْخُلُفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ، عضُّوا عَلَيْهَا بالنَّواجِذِ، وإِيَّاكُمْ ومُحْدثَاتِ الأُمُورِ فَإِنَّ كُلَ بِدْعَةٍ ضلالَةٌ)) رواه أبو داود، والترمذِي وقال حديث حسن صحيح
((Nakuusieni kumcha Allaah, usikivu na twaa hata ikiwa kiongozi wenu (Au atakayekuamrishen) ni Mtumwa wa Habash. Mtakaoishi miongoni mwenu mtaona ikhtilafu nyingi. Kwa hiyo shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa waliongoka baada yangu. Ziumeni kwa magego (zikamateni kwa nguvu wala msiziache). Na tahadharini na mambo ya uzushi kwani kila bid'ah ni upotofu)) [Abu Daawuwd, At-Trimidhiy kasema Hadiyth Hasan Swahiyh]
Na akasema pia:
((تَرَكْتُ فِيكُمْ مَا اِنْ تَمَسَّكْتُمْ بِهِ لَنْ تَضِلُّوا بَعْدِي اَبَداً كِتَابُ الله وَسُنَّتِي))
((Nakuachieni kile ambacho mkikishikilia hamtapotea abadan baada yangu nacho ni Kitabu cha Allaah na Sunnah zangu)) [Hasan: Imesimuliwa na Maalik katika al-Muwattwa (2/899) na al-Haakim (1/93), kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa). Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika as-Silsilah as-Swahiyhah (Namba 1871)]
Tahadhari na shaytwaan ambaye yumo katika jihadi kubwa ya kuwapotosha watu kwa kuwatoa nje ya Swiraatwul-Mustaqiym (Njia iliyonyooka); alisema kumwambia Allaah ('Azza wa Jalla):
قَالَ فَبِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأَقْعُدَنَّ لَهُمْ صِرَاطَكَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿١٦﴾
(Ibliys) Akasema: “Basi kwa kuwa Umenihukumia kupotoka, nitawakalia (waja Wako) katika njia Yako iliyonyooka.”
ثُمَّ لَآتِيَنَّهُم مِّن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَن شَمَائِلِهِمْ ۖ وَلَا تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَاكِرِينَ ﴿١٧﴾
“Kisha nitawaendea mbele yao na nyuma na kuliani kwao na kushotoni kwao, na wala Hutopata wengi wao wenye kushukuru.” [Al-A’raaf: 16-17]
WabiLLaahi At-Tawfiyq